LIVE STREAM ADS

Header Ads

Uingereza yaridhishwa na Uhuru wa Vyombo vya Habari Tanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Balozi ya Uingereza nchini Tanzania Bwana David Concar amefanya ziara kwenye ofisi za Klabu ya Waandishi wa Habari ya Mkoa wa Mwanza (MPC) na kufanya mazungumzo mafupi juu ya hali ya utendaji kazi wa vyombo vya habari nchini.

Balozi Concar amewasili katika ofisi za MPC Machi 21, 2022 na kupokelewa na Mwenyekiti wa MPC Edwin Soko na kisha kupewa kwa ufupi historia na majukumu ya chama hicho.

Pia Balozi alifanya mkutano na waandishi wa habari na kuzungumzia masuala mbalimbali ikiwemo kuimarika kwa uhuru wa vyombo vya habari nchini Tanzania katika kipindi cha mwaka mmoja wa Rais Samia Suluhu Hassan.

"Ni vyema MPC kwenye mpango kazi wake ikaongeza jukumu la kuripoti habari zinazowahusu usawa wa kijinsia na haki za wanawake na watoto" alisema Balozi Concar.

Juu ya mzozo wa vita nchini Ukraine. Balozi alieleza kuwa nchi yake inajikita zaidi kwenye kutoa misaada ya kibinadamu na inaamini kuwa uvamizi wa Urusi dhidi ya Ukraine haukuwa wa haki na ndiyo maana mataifa mengi yanapaza sauti na kumtaka Rais Putin wa Urusi kusitisha vita hivyo.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko amemshukuru Balozi Concar kwa ziara yake hivyo na kusisitiza kuwa bado kuna uhitaji kwa Serikali ya Uongereza kuwa na programu maalumu za kubadilishana ujuzi kati ya waandishi wa habari wa taifa hilo na Tanzania.

"Kwa mwaka mmoja wa utawala wa Rais Samia kumekuwa na uimarikaji wa uhuru wa vyombo vya habari" alisema Soko.

Hii ni ziara ya pili kubwa ya mabalozi kuitembelea MPC ambapo ziara ya kwanza ilikuwa mwezi Disemba 2021 ambapo Balozi wa Marekani nchini Tanzania, Donald Wright aliitembelea MPC na kufanya mazungumzo na viongozi wake pamoja na mkutano na wanachama wa MPC.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.