LIVE STREAM ADS

Header Ads

Siku 365 za Rais Samia: Bilioni 50 zatekeleza miradi ya maendeleo Misungwi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Rais Zaidi ya shilingi bilioni 50 zimetolewa na Serikali ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Hayo yameelezwa Machi 30, 2022 na Mkuu wa Wilaya hiyo, Veronica Kessy wakati akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa kipindi cha Siku 365 (mwaka mmoja) tangu Rais Samia aingie madarakani.

DC Kessy amebainisha kuwa fedha hizo zimetekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ya afya, elimu, maji miundombinu ya barabara na umeme na hivyo kumshuruku Rais Samia kwa kutoa fedha hizo kwa ajili ya kuwaletea wananchi maendeleo.

“Tangu nchi ipate Uhuru hatujawahi kupokea fedha nyingi za maendeleo kiasi hiki ndani ya mwaka mmoja hivyo tunamshukuru Rais Samia kwa kutuletea fedha hizi na hakika anaendelea kuupiga mwingi na sisi Misungwi tutaendelea kuupiga mwingi pia katika maendeleo” amesema DC Kessy wakati.

Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Candida Ignatio akitoa salamu kwenye hafla hiyo kwa niaba ya Katibu Tawalama Mkoa Mwanza, Ngusa Samike amewapongeza viongozi wilayani Misungwi kwa ushirikiano na umoja wao wa kuchapa kazi ikiwa ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia za kuwaletea watanzania maendeleo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika kipindi cha siku 365 za Rais Samia Suluhu Hassan akiwa madarakani.
Watumishi na wakazi wa Misungwi wakifuatilia hafla hiyo. 
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy akiwa na viongozi mbalimbali akikata keki kama ishara ya kusherehekea mafanikio ya siku 365 za Rais Samia Suluhu Hassan pamoja na siku yake ya kuzaliwa mwaka huu 2022 aliyoiadhimisha hivi karibuni.
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Veronica Kessy akiwalisha keki viongozi mbalimbali kwenye hafla hiyo.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.