LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kamatiya Bunge yaridhishwa na Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo Misungwi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LACC), ikiongozwa na Mwenyekiti wake Seleman Zedi imekagua utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza na kuridhishwa na miradi hiyo.

Miongoni mwa miradi iliyokaguliwa na Kamati hiyo ni pamoja na ujenzi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya Misungwi (pichani juu) ambao umekabilika na kuanza kutumika na hivyo kurahisisha utoaji huduma kwa wananchi huku likiongeza wigo kwa viongozi na wataalamu wa Halmashauri hiyo kuwahudumia wananchi kwa ufanisi zaidi.

Kamati hiyo pia imekagua ujenzi wa maabara katika Shule ya Sekondari  Sanjo ambayo ujenzi wake umegharimu shilingi milioni 117 ambapo Serikali imechangia shilingi milioni 60 huku wananchi wakichangia fedha na nguvu kazi kiasi cha shilingi milioni 57 na hivyo Kamati kufurahishwa na jitihada hizo.

Katika hatua nyingine Kamati hiyo imeridhishwa na ujenzi wa Hospitali mpya ya Wilaya Misungwi ambayo imeanza kutoa huduma kwa wananchi ambapo hadi sasa imekamilika kwa asilimia 90 huku kiasi cha shilingi milioni 800 kikitumika kati ya shilingi bilioni 1.5 zilizotengwa kukamilisha ujenzi wake.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LACC), Seleman Zedi (wa pili kulia) akiwasili katika Hospitali ya Wilaya Misungwi kukagua mradi huo.
Mwonekano wa jengo la wagonjwa wa nje katika Hospitali ya Wilaya Misungwi.
Hospitali mpya ya Wilaya Misungwi tayari imeanza kutoa huduma kwa wananchi hususani wagonjwa wa nje.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari Sanjo wilayani Misungwi wakiwa kwenye maabara mpya iliyojengwa shuleni hapo.

No comments:

Powered by Blogger.