LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mwanza awasilisha mafanikio ya Rais Samia, Siku 365

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel Aprili 06, 2022 amewasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo katika kipindi cha siku 365 (mwaka mmoja) tangu Rais Samia Suluhu Hassan aingie madarakani.
Mhandisi Gabriel ametumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya ukamilishaji wa miradi ya zamani na kutoa pia fedha kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mipya ikiwemo ya afya, elimu, maji na miundombinu na kwamba Mkoa wa Mwanza utaendelea kusimamia kwa uadilifu utekelezaji wa miradi hiyo na yeyote atakayejaribu kuikwamisha atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.