LIVE STREAM ADS

Header Ads

MWANZA: Benki ya CRDB yafungua tawi jipya Nansio wilayani Ukerewe

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya CRDB imezindua tawi lake jipya katika mji wa Nansio Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza ikiwa ni hatua ya benki hiyo kuendelea kusogeza karibu zaidi huduma za kibenki kwa wananchi kuendana na kaulimbiu yake ya 'Ulipo Tupo'.

Uzinduzi wa tawi hilo lililopo katika jengo la 'Mnasizu Plaza' ulifanyika Ijumaa Mei 13, 2022 mgeni rasmi akiwa ni Mkuu wa Wilaya Ukerewe, Col. Denis Mwila ambaye alisema hatua hiyo itachochea zaidi maendeleo wilayani humo kupitia huduma zitakazotolewa na benki ikiwemo mikopo.

DC Mwila aliwahimiza wananchi kuchanamkia fursa zitakazotokana na ufunguzi wa tawi la CRDB wilayani Ukerewe hususani mikopo akisema "watu wengi walioendelea walikopa, hata nchi zilizoendelea zina madeni, kwa hiyo ninachowaomba ndugu zangu msiogope kukopa ili kujiendeleza kiuchumi".

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly alisema kabla ya ufunguzi wa tawi hilo, wateja wa Benki hiyo walikuwa wakipata huduma kupitia mawakala wakubwa 32 walio wilayani Ukerewe ambapo kwa Kanda ya Ziwa inayojumuisha mikoa ya Mwanza, Kagera, Simiyu na Mara ina matawi 37 na mawakala 1,300. 

"Tulikuwa na changamoto ya kupata huduma za kibenki ikiwemo kufungua akaunti hapa Ukerewe, ila sasa tunafurahi benki ya CRDB imefungua tawi lake hivyo tunashukuru sana" amesema Chitang'onya Makenena ambaye ni mkazi wa Ukerewe wakati wa hafla ya ufunguzi wa tawi la CRDB Nansio.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe mkoani Mwanza, Col. Denis Mwila (wa pili kushoto) akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa tawi la Benki ya CRDB Nansio wilayani humo. Viongozi wengine walioshiriki ni pamoja na Kaimu Mkurugenzi Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly (wa tatu kulia) na Meneja wa tawi hilo, Gilman Segesa (wa pili kulia).
Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Col. Denis Mwila (wat tatu kushoto) na viongozi mbalimbali akiwemo Kaimu Mkurugenzi Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly (wa nne kulia) wakifurahia hafla ya uzinduzi benki ya CRDB tawi la Nansio wilayani Ukerewe.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Col. Denis Mwila akipata maelezo kuhusiana na huduma zinazotolewa na Benki ya CRDB baada ya kufungua tawi la Benki hiyo mjini Nansio.
Kaimu Mkurugenzi Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Col. Denis Mwila (wa pili kushoto) kuhusiana na huduma zinazotolewa na Benki hiyo.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Col. Denis Mwila (wa pili kulia) akipata ufafanuzi wa huduma mbalimbali zinazotolewa na Benki ya CRDB baada ya kufungua tawi la Benki hiyo katika Mji wa Nansio.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Col. Denis Mwila akizungumza kwenye ufunguzi wa Benki ya CRDB tawi la Nansio ambapo ametoa rai kwa Benki hiyo kuendelea kupanua huduma zake katika visiwa mbalimbali wilayani Ukerewe ili kuendana na kauli mbiu yake isemayo "Ulipo Tupo".
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Col. Denis Mwila akizungumza kwenye hafla hiyo.
Kaimu Mkurugenzi wa Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly amesema ufunguzi wa tawi la benki hiyo katika mji wa Nansio wilayani Ukerewe utaondoa adha waliyokuwa wakiipata wananchi kwa kusafiri umbali mrefu hadi jijini Mwanza kufuata huduma za kifedha ikiwemo mikopo yenye masharti nafuu inayotolewa na benki hiyo ambapo sasa huduma zote zitapatikana Nansio.
Kaimu Mkurugenzi Benki ya CRDB Kanda ya Ziwa, Japhary Hassanaly amesema tayari benki hiyo imepunguza riba za mikopo ya wakulima kutoka asilimia 18 hadi asilimia 09 na kwamba iko kwenye mikakati ya kupunguza riba kwenye mikopo ya wafanyabiashara.
Meneja wa CRDB Tawi la Nansio wilayani Ukerewe, Gilman Segesa akizungumza kwenye hafla hiyo ambapo amewahakikishia wateja wa CRDB upatikanaji wa huduma bora katika tawi jipya la Nansio.
Meneja wa CRDB Tawi la Nansio wilayani Ukerewe, Gilman Segesa (wa nne) akiwatambulisha wafanyakazi wa Benki hiyo tawi la Nansio na kuwahimiza wananchi kuwatumia kupata huduma stahiki za kibenki.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Col. Denis Mwila (wa watu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa CRDB pamoja na Kamati ya Usalama wilayani Ukerewe.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Col. Denis Mwila (wa watu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Col. Denis Mwila (wa watu waliokaa) akiwa kwenye picha ya pamoja na wateja wa Benki ya CRDB baada ya ufunguzi wa tawi la CRDB Nansio.

No comments:

Powered by Blogger.