LIVE STREAM ADS

Header Ads

MPC na UTPC waadhimisha Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari 'RC Mwanza achangia ujenzi wa ofisi'

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel ameahidi kufanya kazi bega kwa bega na waandishi wa habari huku akiwahakikishia mazingira huru ya kufanyia kazi ili kwa pamoja kusaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo mkoani humo

Pia Mhandisi Gabriel amesisitiza kuwa waandishi wa habari wana uhuru wa kupata taarifa wakati wowote wanapozihitaji katika ofisi na taasisi za umma kwani ni jukumu lao kupata taarifa hizo na kuwahabarisha wananchi na ikitokea wamenyimwa taarifa wamjulishe ili achukue hatua.

Mhandisi Gabriel ameyasema hayo Mei 27, 2022 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani ngazi ya Mkoa Mwanza yakiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) kwa kushirikiana na Muungano wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

Mhandisi Gabriel amesema waandishi wa habari wana wajibu mkubwa wa kuchochea amani na maendeleo kupitia kalamu na sauti zao na hivyo kuwahimiza kutimiza wajibu wao kwa weledi kwa lengo la kulisaidia taifa huku akiwasihi kujiendeleza kielimu ili kuendana na mabadiliko ya dunia.

Amesema Mwanza ni Mkoa wa kimkakati ukiwa na fursa mbalimbali ikiwemo uwekezaji na utalii na hivyo kuomba waandishi wa habari kusaidia kutangaza fursa hizo ili kuvutia wawekezaji zaidi pamoja na watalii na kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan ambaye tayari ametangaza vivutio vya Taifa kupitia filamu ya Royal Tour.

Kuhusu changamoto ya ukosefu wa jengo la ofisi za waandishi wa habari mkoani Mwanza, Mhandisi Gabriel ameahidi kushirikiana na MPC kutafuta wadau kwa ajili ya kusaidia ujenzi wa ofisi ambapo ameahidi kutoa shilingi milioni tano kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo.

Katika hatua nyingine Mhandisi Gabriel amesema waandishi wa habari ambao wamejiajiri wana fursa ya kuunda vikundi kuanzia watu watano na kunufaika na mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri kupitia mapato ya ndani akisema yuko tayari kukakikisha suala hilo linatekelezeka bila ubaguzi.

Mhandisi Gabriel ametoa rai kwa waandishi wa habari kuhamasisha wananchi kujiandaa na kushiriki kikamilifu kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi inayotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022 na pia kutoa ushirikiano kwa makarani kwenye zoezi hilo.

Awali Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko amesema hali ya uhuru wa vyombo vya habari nchini imekuwa ya kuridhisha na kutokana na marekebisho ya kanuni na sheria za habari pamoja na vyombo vya habari vilivyokuwa vimefungiwa kufunguliwa.

Hata hivyo Soko amesema licha ya mafanikio hayo bado kuna changamoto kwa wamiliki wa vyombo vya habari kuzingatia suala la maslahi kwa waandishi wa habari ili kuwawezesha kutimiza wajibu majukumu yao vyema.

Maadhimisho hayo yametoka na maazimio manne ambayo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari wa Mkoa Mwanza katika nyanja mbalimbali kitaaluma, kuripoti habari za maendeleo ya Mkoa Mwanza, kuandaa mkakati wa kuwawezesha kiuchumi na kukutana kila baada ya miezi mitatu ili kufanya tathmini ya utendaji kazi.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akizugumza na waandishi wa habari pamoja na wadau wa habari kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika Mei 27, 2022 ngazi ya Mkoa Mwanza yakiandaliwa na MPC kwa kushirikiana na UTPC. Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yalifanyika Mei 03, 2022 na mkoani Mwanza yalisogezwa mbele kupisha maadhimisho ya kitaifa yaliyofanyika mkoani Arusha.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC), Edwin Soko akisoma risala kwa niaba ya waandishi wa habari mkoani Mwanza.
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akizungumza kwenye maadhimisho hayo. Waliokaa ni Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (katikati), Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke (kulia) pamoja na Katibu Mkuu MPC, Blandina Alistides (kushoto).
Waandishi wa Habari wakinasa matukio kwenye maadhimisho hayo.
Afisa Mawasiliano na Uratibu UTPC, akitoa salamu zake wakati wa maadhimisho hayo.
Meneja Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Kanda ya Ziwa, Mhandisi Francis Mihayo akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo ambapo amewahimiza waandishi wa habari hususani wa mtandaoni kuzingatia maadili kwenye kazi zao badala ya kukiuka maadili kwa minajili ya kupata watazamaji/ wasomaji.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo ambapo amepongeza ushirikiano uliopo baina ya waandishi wa habari katika kutangaza habari za mkoa Mwanza.
Sheikh wa Mkoa Mwanza, Hassan Kabeke akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Kaimu Meneja wa NSSF Mkoa Mwanza, Flora Nduta akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo ambapo amewahimiza waandishi wa habari kujiunga na mfuko huo wa mafao.
Mwakilishi wa Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza akitoa salamu za jeshi hilo kwenye maadhimisho hayo ambapo ameahidi ushirikiano wa kutosha kwa waandishi wa habari katika kutimiza majukumu yao.
Mwakilishi wa Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa Mwanza akitoa salamu za jeshi hilo kwenye maadhimisho hayo.
Mwanahabari nguli, Paul Mabuga akiwasilisha mada wakati wa maadhimisho hayo.
Mhadhiri Msaidi kutoka Chuo Kikuu cha SAUT Mwanza, Martin Nyoni akiwasilisha mada kuhusu usalama wa waandishi wa habari mtandaoni.
Mratibu wa MPC akitoa salamu zake wakati wa maadhimisho hayo.
Mweka Hazina wa MPC ambaye pia ni Mjumbe UTPC, Paulina David akitoa salamu zake wakati wa maadhimisho hayo.
Mjumbe MPC, Alphone Tonny akiongoza mjadala wakati wa maadhimisho hayo.
Makamu Mwenyekiti wa Shirikisho la Umoja wa Machinga Tanzania (SHIUMA) Mkoa Mwanza, Joseph Mwita akitoa salamu za shirikisho hilo kwenye maadhimisho hayo.
Meneja wa TCRA Kanda ya Ziwa Mhandisi Francis Mihayo (katikati), Mwenyekiti MPC Edwin Soko (kulia) na Mjumbe wa MPC Alphonce Tonny wakifuatilia maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (wa pili kushoto), Mwenyekiti MPC Edwin Soko (wa pili kulia), Sheikh wa Mkoa Mwanza Hassan Kabeke (kulia) na Katibu Mkuu MPC Blandina Alstides (kushoto) wakifuatilia maadhimisho hayo.
Katibu wa Mkuu wa Mkoa Mwanza, Matia Levi (kulia) akiwa na wadau mbalimbali wa habari mkoani Mwanza kwenye maadhimisho hayo.
Kutoka kushoto ni Mratibu MPC, Mweka Hazina MPC Paulina David na Katibu Mkuu MPC Blandina Alstides.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel (wa pili kushoto) akiwangoza waandishi wa habari na wadau wa habari kuwakumbuka waandishi wa habari wa Mkoa Mwanza waliopoteza maisha kwenye ajali wakati wakielekea kwenye majukumu wilayani Ukerewe.
Waandishi wa habari jijini Mwanza wakiwakumbua wenzao waliopoteza maisha kwenye ajali wakati wakielekea kwenye majukumu wilayani Ukerewe.
Waandishi wa habari jijini Mwanza wakiwakumbua wenzao waliopoteza maisha kwenye ajali wakati wakielekea kwenye majukumu wilayani Ukerewe.
Taswira wanahabari na wadau wa habari wakiwa katika ukumbi wa Nyakahoja jijini Mwanza kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika Mei 27, 2022 kwa ngazi ya Mkoa Mwanza yakiandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa Mwanza (MPC) kwa kushirikiana na Umoja wa Klabu za Waandishi wa Habari Tanzania (UTPC).

No comments:

Powered by Blogger.