LIVE STREAM ADS

Header Ads

RC Mwanza awaahidi neema Wauguzi na Wakunga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel amewaahidi wakunga na wauguzi kwamba Serikali mkoani humo itashughulikia changamoto zinazowakabili ili kuwawezesha kutimiza wajibu wao kwa weledi.

Mhandisi Gabriel ameyasema hayo Mei 26, 2022 wakati akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Wauguzi duniani yaliyofanyika kwa ngazi ya Mkoa Mwanza katika Kituo cha Afya Buzuruga wilayani Ilemela.

Amemwagiza Katibu Tawala Mkoa Mwanza (RAS) kukutana na Mganga Mkuu Mkoa Mwanza (RMO) pamoja na Wakurugenzi wa Halmashauri ili kutafuta mwarobaini wa madai ya wauguzi na wakunga mkoani Mwanza ikiwemo posho la sare pamoja na masaa ya ziada kazini.

Mhandisi Gabriel ameongeza kuwa tayari Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan inaendelea na jitihada za kuajiri watumishi wa afya wakiwemo wakunga na wauguzi ili kukabiliana na uhaba uliopo huku ikiboresha pia maslahi yao kwa kuongeza mshahara kwa asilimia 23.3 na hivyo kuwataka wauguzi na wakunga kufanya kazi kwa weledi na miongozi iliyowekwa na Baraza la Wauguzi na Wakunga Tanzania (TNMC).

Katika hatua nyingine Mhandisi Gabriel ametoa fursa kwa wauguzi na wakunga mkoani Mwanza kufika katika Halmashauri ya Wilaya Ilemela kwa ajili ya kupata mikopo ya viwanja katika eneo tengefu la mji wa kisasa Nyafula jambo ambalo limepokelewa kwa shangwe kwenye maadhimisho hayo huku Mkuu wa Wilaya Ilemela, Hassan Masala akiahidi kusimamia utekelezaji wake.

Awali Katibu wa Chama cha Wauguzi na Wakunga (TANNA) Mkoa Mwanza, Martha Mkinga amesema kuna uhaba wa watumishi kwa asilimia 50 mkoani Mwanza katika kada hiyo hali inayofanya Muuguzi mmoja kuhudumia wagonja kati ya 20 hadi 30 kwa siku badala ya sita hadi nane hatua inayosababisha changamoto kwenye utekelezaji wa majukumu yao kwa weledi.

Kwa upande wake Makamu wa rais wa Chama cha Wauguzi Tanzania (TANNA), Ibrahim Mgoo amewahimiza watumishi wa kada hiyo kufanya kazi kwa bidii bila kutanguliza maslahi mbele na kuhakikisha wanaondoa changamoto ya vifo vya akina mama wanaojifungua, watoto wachanga pamoja na kutoa elimu kwa umma kuhusu magonjwa yasiyoambukiza ikiwemo presha na kisukari kuwaelimisha kuhusu lishe bora na umuhimu wa kufanya mazoezi.

Naye Mganga Mkuu Mkoa Mwanza, Dkt. Thomas Ruttachunzibwa amesema wauguzi na wakunga ni uti wa mgongo na pia jeshi kubwa katika sekta ya afya ambapo wanafikia asilimia 80 ya watumishi wote katika sekta hiyo huku wakiwa ni tegemeo kubwa kwa wataalamu wengine wakiwemo madaktari ambapo wao ndio hukaa na kumhudumia mgonjwa kwa asilimia 100 na hivyo kutumia maadhimisho hayo kuwahimiza kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia weledi na kiapo cha taaluma yao.

Maadhimisho ya Siku ya Wakunga na Wauguzi Duniani yalifanyika Mei 12, 2022 ambapo kitaifa yalifanyika mkoani Kilimanjaro na kwa Mkoa Mwanza yameadhimishwa Mei 26, 2022 yakiambatana na zoezi la utoaji bure huduma za afya kwa wananchi huku kaulimbiu ikiwa ni 'Wauguzi Sauti Inayoongoza, Wekeza Kwenye Uuguzi na Heshimu Haki Kulinda Afya kwa Wote’.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Wilaya Ilemela, Hassan Masala akitoa salamu kwenye maadhimisho hayo.
Mganga Mkuu Mkoa Mwanza, Dkt. Thomas Ruttachunzibwa akizungumza kwenye maadhimisho hayo.
Makamu wa Rais wa Chama cha Wauguzi na Wakunga Tanzania (TANNA), Ibrahim Mgoo akitoa salamu zake kwenye maadhimisho hayo.
Kaimu Muuguzi Mkuu Wilaya ya Ilemela, Grace Kusaya akitoa salamu katika maadhimisho kaka.
Katibu wa TANNA Mkoa Mwanza, Martha Mkinga (kulia) akisoma risala kwa niaba ya wakunga na wauguzi.
Wauguzi na wakunga mkoani Mwanza wakiapa kiapo cha taaluma wakati wa maadhimisho hayo.
Wakunga wakiapa kiapo cha kuzingatia taaluma yao.
Wakunga na Wauguzi wakiapa kuzingatia maadili ya taaluma yao.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akishuhudia Wakunga na Wauguzi wakiapa kiapo cha kuzingatia maadili ya taaluma yao.
Wakunga na Wauguzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo.
Wakunga wakifurahia jambo wakati wa maadhimisho hayo.
Kaimu Mkunga wa Wilaya ya Ilemela, Grace Kusaya (kulia) akimkabidhi zawadi mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel baada ya kuhitimisha hotuba yake iliyotoa faraja kubwa kwa Wakunga na Waugunzi.
Wakunga na Wauguzi wakimtuza Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel baada ya kumaliza hotuba yake.
Wakunga na Wauguzi wakimtuza Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel.
Makamu wa rais wa TANNA, Ibarahim Mgoo (kulia) akimtuza Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel baada ya kuhitimisha hotuba kwenye maadhimisho hayo.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (wa tatu kulia) akikabidhi hati za pongezi wauguzi.

Kaimu Muuguzi Wilaya ya Ilemela, Grace Kusaya akipokea hati ya pongezi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel.

Kaimu Muuguzi Wilaya ya Ilemela, Grace Kusaya.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel (katikati waliokaa) na viongozi mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja na wauguzi na wakunga waliohudhuria maadhimisho hayo.

No comments:

Powered by Blogger.