LIVE STREAM ADS

Header Ads

UVCCM Mwanza wampongeza Rais Samia "Amekuwa Kiongozi Mwenye Ushawishi Duniani"

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Boniphace Zephania Boniphace akizungumza wakati wa kongamano la vijana wa jumuiya hiyo ambapo pamoja na mambo mengine imetoa tamko la kumpongeza Mwenyekiti wa CCM Taifa ambaye pia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa utendaji mzuri wa kazi.
***

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza imempongeza Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa utumishi uliotukuka katika kipindi kifupi cha mwaka mmoja na miezi miwili aliyoliongoza Taifa.

Tamko la pongezi hizo limetolea Alhamisi Mei 26, 2022 jijini Mwanza ambapo zaidi ya makundi mbalimbali zaidi yakiwemo ya machinga na madereva wa daladala jijini Mwanza yamejitokeza kuunga mkono tamko hilo la kumpongeza Rais Samia ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa.

Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Boniphace Boniphace amesema "tumeamua kumpongeza Rais samia kwa kutajwa kuwa miongoni mwa viongozi weye ushawishi mkubwa duniani jambo ambalo limechagizwa na dhamira yake njema ya kukuza Demokrasia, Uhuru wa Vyombo vya Habari, kusisitiza Uwajibikaji na Utawala Bora pamoja na kuongeza uhusiano wa vyama vya upinzani nchini ili kuhakikisha watanzania wanakwenda pamoja katika kukuza uchumi wa Taifa".

Boniphace amesema kuwa wanampongeza pia Rais Samia kwa hatua aliyoichukua ya kuboresha maslahi ya watumishi nchini kwa kuongeza kima cha chini cha mshahara hadi kufikia asilimia 23 huku akiwasihi watumishi kuendelea kufanyakazi kwa weledi ili ongezeko hilo lilete tija katika jamii.

Naye Mwenyekiti wa Soko la Mchafu Kuoga, Amir Ndayambaje ametoa shukurani kwa Rais Samia kwa kuwatengea maeneo rasmi ya kufanyia biashara ambapo kwa sasa wanafanya biashara kwa usalama zaidi ikilinganishwa na zamani walivyokuwa wakiuzia barabarani na kukumbana na changamoto nyingi ikiwemo ya kugongwa na magari.

"Kwa sasa tunatambulika na Serikali pamoja na taasisi mbalimbali za kifedha ambapo tumepata sifa ya kukopesheka, hii yote ni kutokana na kwamba tuna maeneo rasmi ya kufanyia biashara zetu" amesema Ndayambaje.

Aidha Ndayambaje ameeleza kuwa Rais Samia amewaheshimisha machinga kwa kuamua kutoa milioni 10 kila Mkoa kwa ajili ya kujenga ofisi za umoja wao ili wanapokuwa na malalamiko yao wawe na sehemu ya kuyapeleka.

Kwa upande wake Mjarifu Manyasi ambaye ni Mwenyekiti wa Chama cha Madereva Mkoa wa Mwanza (MWAREDA) ameeleza namna ambavyo Rais Samia alivyotoa ruzuku ya Bilioni 100 kwa ajili ya kunusuru upandaji wa mafuta na ana imani kufikia mwezi Juni gharama za mafuta zitakuwa zimepungua na wataendelea kufanya kazi katika mazingira rafiki.

Pia amempongeza kwa namna anavyozidi kuboresha miundombinu katika sekta ya elimu kwa kujenga madarasa kwani hapo awali wanafunzi walikuwa wakiingia shuleni kwa awamu lakini kwa kipindi hiki waemenda kwa awamu moja na wameanza masomo pamoja ambapo pia ametoa wito kwa madereva na makondakita jijini Mwanza kuwapa kipaumbele wanafunzi wanapowakuta kwenye vituo vya daladala ili waweze kuwahi kwenye masomo.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa Mabalozi wa Kujitolea wa Sensa Tanzania, Mansour Jumanne amewahimiza wananchi kushiriki ipasavyo zoezi la Sensa ya Watu na Makazi linayotarajiwa kufanyika Agosti 23, 2022 huku vijana wakiwa mabalozi wa kuhamasisha zoezi hilo ili lifanikiwe kwa asilimia 100 kwani Sensa ni muhimu kwa mipango ya maendeleo ya Taifa huku akimpongeza Rais Samia kwa kuwa miongoni mwa viongozi 100 wenye ushawishi duniani.
Rais wa Awamu ya Sita wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Taifa, Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana, Boniphace Boniphace akitoa tamko la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa miongozi mwa viongozi 100 wenye ushawishi duniani kulingana na orodha iliyotolewa Mei 24, 2022 na jarida la Times.
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Nyamagana, Ramadhani Omary akizungumza wakati wa kongamano hilo la kumpongeza Rais Samia kwa utendaji wake uliotukuta, kuitangaza Tanzania kupitia filamu ya Royal Tour pamoja na kuwa miongoni mwa viongozi 100 wenye ushawishi duniani kwa mujibu wa jarida la Times ambalo pia Machi 13, 1964 lilimtaja Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere kama Kiongozi mwenye Sera za kuibadili Dunia.
Mwenyekiti wa Chama cha Madereva mkoani Mwanza, Mjarifu Manyasi akizungumza wakati wa kongamano hilo la kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan.
Mwenyekiti wa Kundi la Mabalozi wa Kujitolea wa Sensa Tanzania, Mansour Jumanne akieleza umuhimu wa wananchi kushiriki Sensa ya Watu na Makazi Agosti 23, 2022.

No comments:

Powered by Blogger.