LIVE STREAM ADS

Header Ads

PICHA: Maadhimisho ya Siku ya Wauguzi yafanya jijini Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuadhimisha Siku ya Wauguzi Duniani 2022, wauguzi na wakunga mkoani Mwanza wametoa bure huduma za uchunguzi kwa wananchi kuanzia Mei 24-26, 2022 katika Kituo cha Afya Buzuruga wilayani Ilemela.

Huduma zilizotolewa ni pamoja na upimaji wa VVU, shinikizo la damu, macho, uchunguzi wa Saratani ya Shingo ya Kizazi na zoezi la uchangiaji damu kwa hiari ili kuokoa maisha ya wenye uhitaji wa damu.

Siku ya Wauguzi Duniani iliadhimishwa Mei 12, 2022 ambapo kitaifa ilifanyika mkoani Kilimanjaro na kwa Mkoa Mwanza imefanyika Mei 26, 2022 katika Kituo cha Afya Buzuruga kilichopo wilayani Ilemela. 

Pichani ni wauguzi na wakunga mkoani Mwanza wakiwa kwenye maandamano ya amani kutokea viwanja vya maziwa kuelekea Kituo cha Afya Buzuruga kwenye kilele cha maadhimisho hayo yenye kaulimbiu isemayo 'Wauguzi Sauti Inayoongoza, Wekeza Kwenye Uuguzi na Heshimu Haki Kulinda Afya kwa Wote ambapo yamepokelewa na Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Mkoa MwanzA, Mhandisi Roobert Gabriel (wa tatu kulia) akiwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya Ilemela, Hassan Masala (wa pili kulia) kwa ajili ya kupokea maandamano ya wauguzi na wakunga mkoani Mwanza.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhandisi Robert Gabriel akizungumza na wanchi waliojitokeza kupata huduma katika Kituo cha Afya Buzuruga ambapo amesema Rais Samia ameendelea kutoa fedha nyingi kwa ajili ya kuboresha utoaji huduma za afya.

No comments:

Powered by Blogger.