LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi Sengerema watakiwa kukubali fidia kupisha mgodi wa Nyanzaga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa amemtaka Mthamini Mkuu wa Serikali Evelyne Mugasha kumaliza haraka uthaminishaji wa maeneo ya wananchi yaliyochukuliwa na mgodi wa Nyanzaga uliopo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza ili walipwe fidia kupisha shughuli za mgodi.

 Dkt. Kiruswa ametoa kauli hiyo Juni 09, 2022 baada ya kufanya ziara katika mgodi huo unaomilikiwa kwa ubia kati ya Serikali yenye asilimia 16 na kampuni ya OreCop Tanzania Limited kwa asilimia 84 kupitia kampuni ya Sotta Mining.

Aidha Dkt. Kiruswa amesema kuna Haki ya Ardhi na Haki Madini ambapo Wizara ya Madini inasimamia Haki ya Madini na Wizara ya Ardhi inasimamia Haki ya Ardhi na kuongeza kuwa, kazi ya Wizara ya Madini ni kutoa leseni za uchimbaji, kusimamia usalama maeneo ya uchimbaji pamoja na kusimamia mpango wa ushiriki na ushirikishwaji wa wananchi katika Sekta ya Madini. 

Dkt. Kiruswa ameongeza kuwa kuna baadhi ya watu wameendeleza maeneo aidha kwa kujenga nyumba, kupanda mazao na miti katika maeneo mbalimbali baada ya kikomo cha kuendeleza maeneo yanayotegemewa kuchukuliwa na kampuni ya Nyanzaga Mining.

Dkt. Kiruswa amesema ajira zitakazojitokeza katika mgodi huo, watu watakaopewa kipaumbele ni wanakijiji wanaoishi katika eneo linalozunguka mgodi huo.

Sambamba na hayo, Dkt. Kiruswa amesema kati watu 1,606 wanaoishi kuzunguka eneo mgodi  watu 1,455 wamefanyiwa uthaminishaji, watu 1239 sawa na asilimia 85 waliochukua Fomu Namba 3 ya kukubali kulipwa na watu 216 sawa na asilimia 15 wamekataa kuchukua fomu za malipo.

Kwa upande wake, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Dkt. Angelina Mabula amesema Serikali kupitia Mtathmini Mkuu wa Serikali ilifanya tathmini na kubaini maeneo yanayozunguka mgodi wa Nyanzaga yana thamani ya shilingi milioni mbili kwa heka moja.

Pia Waziri Mabula amesema mgodi utalipa mazao yaliopo katika eneo, nyumba, makaburi, posho ya usafiri kwa tani 12 kwa kilometa 20, posho ya miezi 36 kwa ajili  ya kuanzia maisha.

Ameeleza kuwa baadhi ya wananchi wanaoishi katika maeneo yanayozunguka mgodi wa Nyanzaga hawakuwa elimu ya kutosha kuhusu faida watakazozipata baada ya mgodi kuanzia uzalishaji na jitihada za kuwaelimisha zingekuwa zikifanyiwa Ili kutokubali kukwamisha mradi huo.
Na George Binagi (BMG) & Tito Mselem (WM)
Naibu Waziri wa Madini, Dkt. Steven Kiruswa akizungumza na wakazi wa Vijiji vya Buyabu na Sotta vilivyopo Kata ya Igalula Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza wanaotarajiwa kupisha maeneo yao kwa ajili ya shughuli za uchimbaji dhahabu katika mgodi wa Nyanzaga.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Dkt. Angeline Mabula akizungumza kwenye mkutano huo.
Wakazi wa Kata ya Igalula wilayani Sengerema wakifuatilia mkutano huo.
Mthamini Mkuu wa Serikali, Evelyne Mugasha akitoa ufafanuzi kwa wananchi ambapo amesema zoezi la Uthaminishaji limezingatia taratibu zote za kisheria. 
Katibu Tawalama Mkoa Mwanza, Ngusa. samike akitoa salamu za Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel ambapo amesema Serikali ya Mkoa itaendelea kutoa ushirikiano ikiwemo Ili kufanikisha uanzishaji wa shughuli za uzalishajinkatika mgodi wa Nyanzaga kwa amani na usalama. 
Kamishna wa Ardhi Mkoa Mwanza, Elia Kamihanda akizungumza kwenye mkutano huo.
Mkazi wa Igalula wilayani Sengerema, Sengerema Mgwesela akiwasilisha kilio Cha wananchi wenzanke kuomba fidia kuongezeka kutoka shilingi milioni mbili kwa hekali moja Ili kuwawezesha kuhamia maeneo mengine bila adha. 
Mkazi wa Igalula wilayani Sengerema, Manase Athuma akiomba Serikali kuwasaidia thamani ya fidia ya ardhi iongezeke ambapo hata hivyo maombi hayo yameonekana kukinzana na Sheria ya Uthaminishaji na hivyo wananchi kutakiwa kukubali kupokea shilingi milioni mbili kwa hekali moja. 
Wanahabari wakinasa matukio wakati wa mkutano huo. 
Mkazi wa Igalula wilayani Sengerema, Neema Lumala akiomba Serikali kuwasaidia wanawake wakazi wa zoezi la kulipa fidia kwani baadhi ya wanaume huwatelekeza wanapopokea fidia.
Mwakilishi wa mgodi wa Nyanzaga, Delphinius Kaballega amesema taratibu zinaendelea vyema Ili kuhakikisha zoezi la fidia linakwenda vyema pindi litakapoanza. 
Wafanyakazi wa mgodi wa Nyanzaga pamoja na wananchi wakifuatilia mkutano huo.
Wananchi wakifuatilia mkutano huo.
Viongozi mbalimbali meza Kuu akiwemo Waziri wa Ardhi Dkt. Angelina Mabuka na Naibu Waziri wa Madini Dkt. Steven Kiruswa wakiwa kwenye mkutano huo uliolenga kuongeza na wananchi na kuwahimiza kukubali maeneo yao kufanyika tathmini kwa ajili ya kulipwa fidia ili kupisha shughuli za mgodi wa Nyanzaga. 
Viongozi na Watendaji mbalimbali wakifuatilia mkutano huo. 
Wananchi wakiwa kwenye mkutano huo. 
Mkutano ukiendelea.

No comments:

Powered by Blogger.