LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mgodi wa Buckreef washusha neema kwa watanzania

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko ameupongeza mgodi wa dhahabu wa Buckreef kwa kutoa ajira kwa watanzania wanaofanya kazi mbalimbali za uzalishaji wa dhahabu katika mgodi huo 

Dkt. Biteko alibainisha hayo Julai 16, 2022 alipotembelea mgodi huo wa Buckreef mkoani Geita ili kujionea maendeleo ya shughuli za ujenzi na uchimbaji madini ya dhahabu.

Alisema mgodi wa Buckreef umetoa ajira za moja kwa moja 354 kwa watanzania katika nafasi mbalimbali katika mgodi huo.

Alisisitiza wafanyakazi waliopewa ajira katika mgodi huo kuhakikisha wanajenga taswira nzuri kwa kuwa wazalendo na waaminifu katika kazi zao.

Alisema kupitia uaminifu wawekezaji watatoa fursa zaidi kwa Watanzania kuweza kufanya kazi mbalimbali.
Aidha Dkt. Biteko alisisitiza kuwa miradi yote iliyopo kwenye Sekta ya Madini itaendelezwa ili watanzania wanufaike na rasilimali madini na kuongeza Pato la Taifa.

"Matarajio ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan ni kwamba miradi yote ambayo ipo kwenye Sekta ya Madini iweze kuendelezwa" alisisitiza.

Kwa upande wake Mkuu Mkoa wa Geita, Rosemary aliupongeza mgodi wa Buckreef kwa kusimamia usalama kwa wafanyakazi.

Alimuomba Dkt. Biteko kuhakakisha Serikali inaleta wawekezaji wengi mkoani Geita kutokana na mkoa huo kuwa na maeneo mengi ya uwekezaji katika Sekta ya Madini.

Naye Meneja Mkuu wa Mgodi wa Buckreef, Gaston Mujwahuzi alisema wataendelea kuwashirikisha wananchi katika huduma za kijamii kwa ajili ya manufaa ya watu wote.

Alisema shughuli nyingi za manunuzi ya vifaa mbalimbali zinafanyika hapa nchini ili kuhakikisha manufaa ya uwekezaji yanabaki kuwa ya watanzania.

Kampuni ya Dhahabu ya Buckreef ikishirikiana na mbia mwenza Shirika la Madini la Taifa (STAMICO) inajushughulisha na uchimbaji wa madini ya dhahabu. Pia kampuni ya Buckreef inamiliki hisa kwa asilimia 55 na STAMICO inamiliki hisa asilimia 45.
Na Steven Nyamiti, WM

No comments:

Powered by Blogger.