LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jiji la Mwanza laanza ujenzi wa barabara korofi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni Diwani wa Kata ya Mhandu jijini humo (mwenye shati nyeupe) akizungumza wakati wa ziara ya kukagua ujenzi wa barabara ya mawe katika Mtaa wa Maswa Mashariki ili kukabiliana na changamoto iliyokuwepo awali.

Na Hellen Mtereko, Mwanza
Wananchi wa Mtaa wa Maswa Mashariki, Kata ya Mhandu jijini Mwanza wamefurahishwa na ujenzi wa barabara ya Ndama inayojengwa kwa mawe yenye urefu wa mita 400 katika Mtaa huo ambayo itasaidia kuondokana na kero mbalimbali walizokuwa wakizipata kutokana na ubovu wa barabara hiyo. 

Wameyasema hayo Julai 09, 2022 wakati wa ziara ya Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine iliyolenga kukagua ujenzi wa barabara hiyo ambayo ni kiunganishi muhimu kutokea eneo la Ndama barabara kuu ya Nyerere.

Anna Kampala ni mkazi wa Mtaa wa Maswa Mashariki, amesema barabara hiyo imekuwa mbovu kwa takribani miaka 50 hali ambayo ilikuwa ikisababisha adha kubwa hususani msimu wa mvua.

"Wakati wa mvua hali ilikuwa ni mbaya zaidi kwani maji yalikuwa yakituama na kutengeneza mabonde, wagonjwa walikuwa wanapata shida kufika hospitalini sanjari na wazazi kujifungulia njiani, lakini kwa sasa shida zote hizo itakuwa ni historia" amesema Kampala

Kwa upande wake Philipo James ambaye pia pia ni Mkazi wa Mtaa wa Maswa Mashariki amesema kukamilika kwa barabara hiyo KUtasaidia makazi yao kuwa na thamani na kuongeza idadi ya watu watakaokuwa wanaitumia kwa ajili ya shughuli mbalimbali za kijamii.

Naye Mwenyekiti wa Mtaa wa Maswa Mashariki, Rashid kabazi ameishukuru Serikali kwa namna ambavyo wameiangalia barabara hiyo kwa jicho la pili kwani wananchi walikuwa wanapata changamoto wakati wa kupita kwenda sehemu mbalimbali.

Nao baadhi ya mafunzi wanaotekeleza mradi huo akiwemo Hamadi Suleiman wamesema wanakutana na changamoto ya wananchi kupita wakati ujenzi unaendelea na hivyo kukwamisha juhudi za kukamilisha ujenzi mapema.

Awali Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Constantine amesema mradi huo utagharimu zaidi ya milioni 234 na unatarajiwa kukamilika ndani ya wiki moja kuanzia sasa.

Amesema Serikali inazidi kufanya kazi kubwa ya utatuzi wa kero mbalimbali katika sekta ya miundombinu kwa kutoa fedha za kujenga barabara mpya na kukarabati barabara zmbalimbali na Kata ya Igoma, Mhandu tumekuwa wanufaika wa fedha hizo.

Ameongeza kuwa mradi huo unaotekelezwa na kampuni ya Rasu Contractor utawanufaisha wakazi wa Mitaa zaidi ya minne na ni mfululizo wa miradi ya barabara inayoendelea kutekelezwa katika Kata ya Mhandu jijini Mwanza. 
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Ndama inayojengwa kwa kiwango Cha mawe.
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (mwenye shati jeupe) na viongoziakishiriki ujenzi wa barabara ya Ndama.
Mafundi wakiendelea na ujenzi wa barabara ya Ndama jijini Mwanza inayojengwa kwa kiwango Cha Mawe. 
Mstahiki Meya wa Jiji la Mwanza, Sima Costantine (mwenye shati nyeupe) akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wakazi wa Mtaa wa Maswa Mashariki.

No comments:

Powered by Blogger.