LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watoto wanaoishi katika mazingira magumu kuhesabiwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Watoto wasiokuwa na makazi maalum na wanaoishi katika mazingira magumu watahesabiwa katika zoezi la Sensa na Makazi.

Kauli hiyo ilitolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Amina Makilagi wakati akifungua mafunzo ya kuandika habari mwendelezo za Sensa yaliyofanyika tarehe 19/08/2022 jijini Mwanza.

Makilagi alisema maandalizi ya zoezi hilo la Sensa na Makazi limekamilika Kwa asilimia 90 na hakuna kundi litakaloachwa kuhesabiwa.

"Nataka tu nisisitize kuwa Kila mmoja wetu atahesabiwa,watoto wote wa mtaani nao tutawahesabu Kwa kuwa tayari tumeweka mpango maalumu" alisema Makilagi.

Alisema tayari makarani wamezungukia maeneo yote wanapopatikana watoto hao na wataanza kuhesabiwa kuanzia majira ya saa 6:00 usiku kwa kufika katika maeneo ambayo wanalala.

"Kwa kuwahesabu watoto wetu hawa itatisaidia sisi Kama wilaya kujua idadi yao na mahitaji ili tujipange sasa kuwaondoa katika Mazingira magumu waliyopo sasa" alisema Makilagi.

Aliyataja makundi mengine ambayo yatahesabiwa kuanzia saa sita usiku ni waliolala katika nyumba za wageni, wasafiri watakaokuwa kwenye meli pamoja na vituo vya kusafiria.

Akizungumzia mafunzo hayo ya kuandika habari mwendelezo za Sensa, Makilagi aliwataka wanahabari kuendelea kuandika matokeo ya zoezi la Sensa ili wananchi waone umuhimu wake.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari wa Kupiga Vita Matumizi ya Dawa za Kulevya na Uhalifu Tanzania (OJADACT), Edwin Soko aliwataka wanahabari wote waliopata mafunzo hayo kwenda kutekeleza elimu hiyo kwa vitendo.
Na Tonny Alphonce, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.