LIVE STREAM ADS

Header Ads

DC Nyamagana awapiga msasa wananchi umuhimu wa Sensa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wananchi wa Kata ya Buhongwa iliyoko Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza wamejitokeza kupata elimu ya Sensa ya watu na makazi inayotarajiwa kufanyika Agositi 23 mwaka huu.

Elimu hiyo ilitolewa Jumamosi Agosti 20, 2022 na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Amina Makilagi kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika stendi ya daladala Buhongwa.

Akizungumza na wananchi hao, Makilagi alisema Sensa ni muhimu kwa maendeleo ya mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

"Sensa ya watu na makazi katika Wilaya yetu ni faida kwani tutajulikana tupo wangapi na changamoto zote tulizonazo kupitia mpango wa Taifa zinakwenda kutatuliwa" alisema Makilagi

Alieleza kuwa idadi ya watu inaongezeka kila siku hivyo kupitia Sensa ya Watu na Makazi Serikali itapata takwimu sahihi ambazo zitatumika kuwaleta maendeleo.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi.

Aidha Makilagi aliongeza kuwa maandalizi ya Sensa katika Wilaya ya Nyamagana yamekamilika huku akiwaomba na kuwasihi wananchi kuwa tayari kuhesabiwa kwenye zoezi la Sensa ya Watu na Makazi.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Nyamagana, Stanslaus Mbula alisema Sensa ya Watu na Makazi itasaidia kubadilisha taswira ya nchi kutokana na kuboresha miundombinu itakayoendana na idadi ya watu.

Alisema wananchi wengi hawana uhakika wa kupata maji yakutosha kwa siku na wengine hawajawahi kupata maji ya bomba wakiwemo wananchi wa Kata jirani ya Lwanima kutokana na wingi wa watu, kuchoka kwa miundombinu ya maji ambayo imekuwepo kwa muda mrefu.

"Maji yamekuwa ni changamoto sana katika baadhi ya maeneo lakini niwahakikishie maji ya uhakika yatapatikana Aprili 2023 mara baada ya mradi wa maji unaojengwa Sawah kukamilika" alisema Mabula

Taliguli kulwa na Mwajuma Hamis ambao ni miongoni mwa wananchi wa Kata ya Buhongwa walisema kutokana na elimu waliyoipata watakwenda kuwa mabalozi wa kuwaelimisha na kuwahamasisha watu wengine ili washiriki kuhesabiwa katika Sensa.
Baadhi ya wananchi waliojitokeza kwenye mkutano wa hamasa ya Sensa ya Watu na Makazi katika Kata ya Igoma jijini Mwanza. 
Na Hellen Mtereko, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.