Ofisi ya Ardhi Mkoa Mwanza yarahisisha upatikanaji wa Hati
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com

Akizungumza Ijumaa Septemba 09, 2022 kwenye uzinduzi wa kituo jumuhishi cha kutolea hati kilichopo Rock City Mall Manispaa ya Ilemela, Kamishina wa Ardhi Mkoa Mwanza, Elia Kamihanda alisema lengo la kutoa hati hizo ni kuhakikisha kazi zote za urasimishaji wa makazi zinakamilika kwa wakati ifikapo mwaka 2023.
Alisema wameanza kutekeleza maelekezo ya Wizara ya Ardhi ya kuwepo kwa vituo jumuhishi vitakavyosaidia utoaji wa hati kwa haraka ambapo hadi sasa katika Kituo cha Rock City Mall wananchi 55 wamekamilisha taratibu na kupewa hati.
Alisema zoezi hilo la vituo jumuhishi litasaidia kuondoa malalamiko kwa Wananchi ya ucheleweshwaji wa upatikanaji wa hati.
Katika hatua nyingine Kamihanda alisema wamezindua programu ya uuzaji wa viwanja katika Manispaa ya Ilemela ambavyo vimepimwa kwenye utaratibu wa miradi ya kupanga, kupima na kumilikisha ardhi.
Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mipango Miji na Ardhi Manispaa ya Ilemela, Shukrani Kyando alisema Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania imeikopesha Halmashauri hiyo shilingi Bilioni 3.6 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa viwanja ambavyo vimeanza kuuzwa katika eneo la Sangabuye.
Kwa upande wao Yusuphu Manyonyi pamoja na Safia Mkama ambao ni miongoni mwa wananchi waliojitokeza kwenye zoezi la uzinduzi wa kituo jumuishi cha kutolea hati Rock City wamesema utaratibu huo ni mzuri kwani utasaidia kuondoa ucheleweshaji wa upatikanaji wa hati kwa wananchi ambao ulikuwepo awali na kuondoa migogoro isiyo ya yaliza.




Na Hellen Mtereko, Mwanza
No comments: