LIVE STREAM ADS

Header Ads

Serikali yahimiza watoto wote kupatiwa chanjo ya Polio

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma, Remidius Mwema amezindua rasmi zoezi la utoaji wa chanjo ya ugonjwa wa polio kwa awamu ya tatu ambapo wataalamu watapita nyumba kwa nyumba kuhakikisha watoto wanaostahili wanapatiwa chanjo hiyo.

Katika uzinduzi huo uliofanyika kiwilaya katika Zahanati ya Makawa iliyopo Kijiji cha Makawa wilayani humo, DC Mwema aliwataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo kwa kuhakikisha watoto wote walio na umri chini ya miaka mitano wanapatiwa chanjo hiyo muhimu.

Akitoka taarifa ya zoezi hilo, Mganga Mkuu wa Wilaya Dkt. Thomas Samwel alisema Wilaya ya Kongwa inatarajia kutoa chanjo kwa watoto wenye kuanzia miezi 0-59 ambapo katika Wilaya hiyo wanatarajia kuwachanja watoto 93, 596.

Aidha alisema chanjo zipo za kutosha na kwamba lengo la Serikali ni kuwalinda wananchi wake akisema chanjo hiyo inasaidia kuwakinga watoto kupata maambukizi ya ugonjwa wa polio unaosababisha viungo kupooza.
Na Maganga Gwensaga, Dodoma

No comments:

Powered by Blogger.