LIVE STREAM ADS

Header Ads

Zaidi ya watoto Milioni 12 wapatiwa chanjo ya Polio

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Watoto 12,131,049 sawa na asilimia 117.8 wamepatiwa chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa Polio kwa watoto chini ya miaka mitano kati ya watoto 10,295,316 waliolengwa nchini Tanzania.

Waziri wa Afya,Ummy Mwalimu amesema Mei 18 , 2022, Wizara hiyo ilizindua awamu ya pili ya kampeni ya kitaifa ya utoaji wa chanjo ya matone dhidi ya ugonjwa wa Polio.

"Uzinduzi wa kampeni hii ya kitaifa ulifanyika katika viwanja vya Chinangali Park vilivyoko katika Jiji la Dodoma na utekelezaji wake kuendelea kwa siku nne mfululizo kuanzia Mei 18 hadi 21 Mei, 2022 ikihusisha mikoa yote hapa nchini" alisem Ummy.

Ummy alisema kampeni hiyo ililenga kuwapatia chanjo watoto 10,295,316 kwa Tanzania bara.
Alisema Ufanisi wa utoaji wa chanjo hiyo umetofautiana kutoka mkoa mmoja hadi mkoa mwingine kwa asilimia.

"Kwa ngazi ya mikoa, Mkoa wa Ruvuma ulivuka lengo kwa asilimia 131, ikifuatia na Shinyanga asilimia 128, Rukwa asilimia 123, Pwani asilimia 122, Arusha asilimia 122, Mbeya, Geita, Dar es Salaam na Simiyu yote ina asilimia 121" alibainisha Ummy.

Kwa upande wa Singida, Dodoma na Tabora asilimia 118, Kigoma, Njombe, Katavi asilimia 117, Morogoro asilimia 116, Mara, Mtwara, Lindi na Tanga asilimia 115, Kilimanjaro na Mwanza asilimia 114, Manyara na Iringa asilimia 113, Songwe na Kagera asilimia111.

Mwezi Septemba 2022 Tanzania imeingia awamu ya tatu ya utoaji chanjo ya polio kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano ambapo lengo ni kuwafikia walengwa wote ili kuwakinga na ugonjwa wa polio unaosababisha viungo kudumaa.

No comments:

Powered by Blogger.