LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waziri wa Maliasili na Utalii avutiwa na mashindano ya magari Iringa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Moja ya magari ambayo yalishiriki katika mashindano Sao Hill Misitu Auto Cross Tanzania The Royal Tour.
Zawadi mbalimbali.

Na Fredy Mgunda, Iringa
Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana amevutiwa na ubunifu na mawazo mazuri yaliofanywa na shamba la Serikali Sao Hill kwa kuandaa mashindano ya mbio za magari katika msitu huo kwani ni fursa kubwa ya kutangaza vivutio mbalimbali vya utalii vilivyopo kwenye shamba hilo.

Balozi Dkt. Chana aliyasema Hayo wakati akizungumza kwa njia ya simu katika Mashindano Sao Hill Misitu Auto Cross Tanzania The Royal Tour kwa kushirikiana Iringa Motorsports Club Tanzania kwa ubunifu huo kwani unaumuhimu mkubwa katika masuala mazima ya kutangaza utalii.

"Haya nimaelekezo ya Rais wetu Samia Suluhu Hassan ambaye alituelekeza kuendelea kubuni vyanzo mbalimbali vya utalii kwani ndio chanzo kimoja wapi katika masuala mazima ya utalii wa aina hiyo wa mashindano ya mbio za mahari au Rally katika misitu yetu ambavyo tunaihifadhi mwenye maeneo yetu " alisema Balozi Dkt. Chana.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Shamba la Sao Hill, Lucas Sabida alisema wameandaa mashindano mafupi ya mbio za mahari lakini wanampango wa kuandaa mashindano makubwa zaidi.

Alisema lengo la mashindano hayo ni kuendelea kujitangaza kama shamba la TFS kwa ajili kutangaza utalii wa ikolojia na nyuki kupitia utalii wa michezo wa mbio za Magari kutokana na mwitikio kuwa mkubwa kwao wananchi.

Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Saad Mtambule alisema kuwa wilaya hiyo ina misitu msingi ambapo wanaziadi ya hekta 100,000 ambayo inatumiwa kwa ajili ya uzalishaji wa mbao pamoja na bidhaa zingine kama 'Marine Board', mirunda na nguzo za umeme.

Alisema mazao hayo wamekuwa wakiyatumia na kuwasaidia kwa uchumi na mapato kwa mustakabali wa jamii lakini kupitia program ambayo ilianzishwa na Rais wa Jamhuria ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan The Royal Tour.

No comments:

Powered by Blogger.