LIVE STREAM ADS

Header Ads

USAID yaipongeza Kongwa kwa usimamizi mzuri sekta ya afya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi wa Afya kutoka shirika la USAID hapa nchini, Bi. Anne Murphy ameoridhishwa na zoezi la utoaji wa chanjo ya Uviko-19 na shughuli nyingine zinazofadhiliwa na shirika hilo katika Wilaya Kongwa mkoani Dodoma.
Pongezi hizo alizitoa Sept 13, 2022 muda mfupi baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa zoezi la utoaji wa chanjo ya Uviko-19 katika Wilaya ya Kongwa ukiwa ni mmoja Kati ya mradi unayofadhiliwa na shirika hilo.

Mbali na hilo, Mkurugenzi huyo alipongeza ushirikiano mkubwa baina ya viongozi wa Wilaya akisema kuwa amefurahishwa zaidi na umoja huyo.

“Tumefurahishwa sana na ushirikiano wenu na bidii katika kazi, tuna mategemeo makubwa zaidi na nyie nasi tunaahidi kuendelea kushirikiana nanyi” alisema Bi. Anne.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Kongwa, Mhe. Remidius Mwema aliwashukuru USAID kwa ushirikiano ambao wamekuwa wakiutoa na kuahidi kuendelea kushirikiana na wadau kufanikisha malengo katika sekta ya afya.

“Niwahakikishie Serikali, inayoongozwa na Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan itaendelea kushirikiana na USAID katika utekelezaji wa afua mbalimbali za sekta ya afya wilayani hapa” alisema Mwema.

Akiwa wilayani humo Bi. Anne alitembelea Kituo cha afya cha Ugogoni na kushuhudia zoezi la utolewaji wa chanjo ya Uviko likiendelea.

Tangu mwaka 2019 hadi sasa Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 6.23 kwa Wilaya ya Kongwa na kuwezesha ujenzi wa Vituo vipya vitano vya afya (Chamkoroma, Pandambili, Chitego, Songambele na Sejeli) pamoja na upanuzi wa Vituo ya afya wiwili ( Kibaigwa na Mkoka) na umaliziaji wa Zahanati Tisa.

Jitihada za Serikali ni kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora za afya na kuwapunguzia adha ya kutembea umbali mrefu kufuata huduma hii.

Kwa kipindi kirefu sasa USAID wamekuwa ni wadau muhimu katika kufanikisha utekelezaji wa Miradi mbalimbali katika Sekta ya Afya hapa nchini ikiwa ni pamoja na Wilaya ya Kongwa.

Pamoja na mambo mengine, USAID kupitia JHPIEGO wamekuwa wadau muhimu kwa kushirikiana na Serikali katika kufanikisha huduma za chanjo za kawaida na UVIKO-19
wilayani humo.
Na Maganga Gwensaga, Dodoma
Ugeni wa USAID ukiwa katika kituo cha afya Ugogoni wilayani Kongwa.
Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Mwema(Mwenye suti) na Bi. Anne Murphy Mkurugenzi wa afya kutoka USAID(Kushoto).
Mhe. Remidius Mwema Mkuu wa Wilaya ya Kongwa.
Bi. Anne Murphy Mkurugenzi wa afya kutoka USAID.
Bi. Alice Christensen Mkurugenzi wa Shirika la JHPIEGO nchini.

1 comment:

  1. However, be careful with on line casino websites that you have got} never heard of before. It's additionally helpful to learn critiques from different gamers, as they may have firsthand expertise with potential issues corresponding to gradual funds or unresponsive buyer help. Taking some time to analysis these elements can ultimately result in 바카라사이트 a greater and more enjoyable digital playing expertise. Different gamers have totally different preferences phrases of|in relation to} making online funds. Thus, we all the time make sure that|be positive that} our casinos settle for broad variety|all kinds} of payment strategies, so find a way to|you presumably can} select the one you're most comfortable with.

    ReplyDelete

Powered by Blogger.