LIVE STREAM ADS

Header Ads

Shirika la DSIK Tanzania lashauri somo la Fedha kuingizwa kwenye mitaala ya elimu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Online Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la DSIK Tanzania limeishauri Serikali kupitia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kuingiza somo la fedha kwenye mitaala wa elimu na kuanza kufundishwa katika Shule za Msingi na Sekondari hatua itakayosaidia kuwa na jamii yenye maamuzi sahihi kuhusu masuala ya kifedha.

Mkufunzi wa  Elimu ya Fedha kutoka shirika hilo, CPA. Rukia Amini ametoa rai hiyo Oktoba 28, 2022 wakati akizungumza na wanafunzi wanaounda Klabu ya Akiba katika Shule ya Msingi Advent iliyopo jijini Mwanza ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya Wiki ya Akiba Duniani.

Amesema kwa sasa elimu ya fedha nchini inafundishwa mashuleni kama somo la ziada jambo ambalo halitiliwi mkazo ipasavyo na hivyo shirika hilo ambalo linajihusisha na utoaji elimu ya fedha kwa makundi mbalimbali ikiwemo wanafunzi, waalimu na wajasiriamali linaona ipo haja ya somo hilo kuingizwa rasmi kwenye mitaala ya elimu ya msingi na sekondari.

CPA. Amini amesema somo la elimu ya fedha litawajenga wanafunzi wangali bado wadogo ili kufanya maamuzi sahihi kwa baadae hususani kutambua umuhimu wa kuweka akiba, kufanya matumizi sahihi ya fedha na kusimamia kwa ufanisi shughuli za uzalishaji mali kwa kuweka kumbukumbu sahihi za mapato na matumizi. 

Ushauri huo umetolewa wakati mwafaka ambapo Serikali inaendelea kupokea maoni ya wadau mbalimbali wa elimu kwa ajili ya maboresho ya mitaala ya elimu nchini kwa lengo la kuwasaidia wahitimu kuwa na ujuzi kuajiriwa ama kujiajiri.

Nao baadhi ya wanafunzi wa shule hiyo ambao ni Helga Samwel, Khajira Mussa na Masirori Nathaniel wamesema elimu elimu ya fedha wanayoipata kupitia klabu ya akiba shuleni hapo imewajengea hamasa ya kujiwekea akiba na kujifunza kwa vitendo shughuli za uzalishaji mali ikiwemo kutengeneza sabuni za maji pamoja na kuanzisha kilimo cha bustani ya mboga mboga hatua inayowajenga kwa maisha ya baadae.

Shirika la DSIK lilianzishwa na umoja wa mabenki ya akiba Ujerumani mwaka 1924 kwa lengo la kutoa elimu ya fedha katika jamii hususani umuhimu wa kuweka akiba baada ya kubainika uchumi wa familia nyingi ulikuwa natetereka kutokana na kukosa elimu hiyo. Nayo Wiki ya Akiba Duniani huadhimishwa kila mwaka wiki ya mwisho ya mwezi Oktoba ikilenga kuhamasisha jamii kuweka akiba kwa manufaa ya baadae hivyo shirika la DSIK linaadhimisha wiki hiyo kwa kuwa ni mdau mkubwa wa masuala ya fedha.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkufunzi wa Elimu ya Fedha kutoka shirika la DSIK Tanzania, CPA. Rukia Amini (katikati) akizungumza kwenye maadhimisho ya Wiki ya Akiba Duniani 2022 yaliyofanyika katika Shule ya Msingi Advent iliyopo jijini Mwanza.
Wanafunzi wa Klabu ya Akiba katika Shule ya Msingi Adent jijini Mwanza wakionesha igizo lenye kuhamasisha uwekaji akiba.
Wanafunzi wa Klabu ya Akiba katika Shule ya Msingi Adent jijini Mwanza wakionyesha jumbe mbalimbali za zinazohusiana na elimu ya fedha.
Wanafunzi wa Klabu ya Akiba katika Shule ya Msingi Adent jijini Mwanza wakionyesha bidhaa za sabuni ya maji wanazotengeza kama sehemu ya mafunzo waliyopata kupitia Klabu ya Akiba shuleni hapo.
Mkufunzi wa  Elimu ya Fedha kutoka shirika hilo, CPA. Rukia Amini (kulia) akinunua sabuni ya maji iliyotengenezwa na wanafunzi wa Shule ya Msingi Advent jijini Mwanza.
Wanafunzi wa Klabu ya Akiba katika Shule ya Msingi Adent jijini Mwanza.
Wanafunzi wa Klabu ya Akiba katika Shule ya Msingi Adent jijini Mwanza.
Mwakilishi kutoka Shirika la DSIK Ujerumani, Fabian Partsch akitoa salamu zake.
Wadau wakishuhudia bustani ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Avent jijini Mwanza.
Bustani ya mbogamboga inayosimamiwa na wanafunzi wa Klabu ya Akiba katika Shule ya Msingi Adent jijini Mwanza.
Mwanachama wa Klabu ya Akiba katika Shule ya Msingi Avent jijini Mwanza, Helga Samwel akieleza kuhusu umuhimu wa elimu ya fedha.
Mwanachama wa Klabu ya Akiba katika Shule ya Msingi Avent jijini Mwanza, Khajira Mussa akieleza elimu ya fedha itakavyomsaidia maishani.
Mkufunzi wa Elimu ya Fedha kutoka shirika la DSIK Tanzania, CPA. Rukia Amini amesema shirika hilo limeunda Klabu za Akiba katika Shule zaidi ya 90 mkoani Mwanza kwa ajili ya kuwafundisha wanafunzi elimu ya fedha kupitia masomo ya ziara na hivyo kushauri somo hilo kuingizwa kwenye mtaala wa elimu nchini.
Shirika la DSIK Tanzania limekabidhi pia mabegi, madaftari, kalamu pamoja na taulo za kike kwa wanafunzi wanaounda Klabu ya Akiba katika Shule ya Msingi Avent ili kuwarahisishia usomaji wa elimu ya fedha.

No comments:

Powered by Blogger.