LIVE STREAM ADS

Header Ads

Askofu mpya AICT Dayosisi ya Geita aanza rasmi majukumu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Askofu wa kanisa la AICT Dayosisi ya Geita, Askofu Reuben Ng'wala ameanza rasmi majukumu yake baada ya kusimikwa na kuwekwa wakfu katika ibada iliyoongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa hilo, Askofu Mussa Magwesela. 

Askofu Ng'wala anachukua nafasi ya Askofu Magwesela aliyechaguliwa kuwa Askofu Mkuu AICT. Mgeni rasmi kwenye ibada hiyo iliyofanyika Jumapili Disemba 11, 2022 katika kanisa la AICT Yeriko mjini Geita alikuwa Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko.
Askofu Mkuu Kanisa la AICT, Askofu Mussa Magwesela akiongoza ibada ya kumsimika na kumweka wakfu Askofu wa kanisa hilo jimbo la Geita, Askofu Reuben Ng'wala.
Askofu wa tatu wa Kanisa la AICT Jimbo la Geita, Askofu Reuben Ng'wala.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akizungumza kwenye ibada ya kumsimika na kumweka wakfu Askofu wa Jimbo wa Kanisa la AICT Jimbo la Geita, Askofu Reuben Ng'wala.
Waziri wa Madini, Dkt. Doto Biteko akizungumza kwenye ibada ya kumsimika na kumweka wakfu Askofu wa Jimbo wa Kanisa la AICT Jimbo la Geita, Askofu Reuben Ng'wala.
Askofu wa Kanisa la AICT Jimbo la Geita, Askofu Reuben Ng'wala.
Tazama BMG TV hapa chini
SOMA>>> 

No comments:

Powered by Blogger.