LIVE STREAM ADS

Header Ads

Waalimu watambua mchango wa Shirika la KIVULINI

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Mkoa Mwanza kimetoa cheti cha pongezi kwa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wa shirika hilo katika kuwajengea uwezo waalimu hususani wanawake kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Cheti hicho kilikabidhiwa kwa Mkurugenzi wa shirika la KIVULINI Disemba 09, 2022 jijini Mwanza wakati wa hafla ya kufunga programu ya CWT Mkoa Mwanza ya kuwajengea uwezo waalimu wanawake iliyodumu kwa kipindi cha mwaka 2021/22.

Mwenyekiti wa CWT Mkoa Mwanza, Mwl. Lameki Mahewa alisema shirika la KIVULINI limekuwa mstari wa mbele kuwajengea uwezo/ uelewa waalimu wanawake kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia katika mazingira ya nyumbani na kazini na hivyo kuwaweka salama kutimiza kwa weledi majukumu yao.

Naye Katibu Kitengo cha Waalimu Wanawake Mkoa Mwanza, Mwl. Rachel Malifedha alisema shirika la KIVULINI limewanusuru waalimu hususani wanawake kutoka kwenye mtego wa ukatili wa kijinsia ikiwemo vipigo, kudhulumiwa mali, fedha na mikopo umiza na sasa hawako tayari kuvumilia tena vitendo hivyo kama awali kwani kila mmoja yuko tayari kuvifichua.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema waalimu wengi walikuwa wakipitia mazingira ya ukatili wa kijinsia katika mahusiano ya ndoa lakini wanavumilia wakihofia jamii itawachukuliaje jambo ambalo si sahihi kwani madhara yake yanaweza kusababisha kujeruhiwa ama kuuawa hivyo shirika hilo limewasaidia kutonyamazia tena vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Mkoa Mwanza, Mwl. Lameki Mahewa akizungumza kwenye hafla ya kufunga programu ya kuwajengea uwezo waalimu wanawake kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia iliyodumu katika kipindi cha mwaka 2021/22.
Katibu Kitengo cha Waalimu Wanawake Mkoa Mwanza, Mwl. Rachel Malifedha akizungumza kwenye hafla ya kufunga programu ya kuwajengea uwezo waalimu wanawake ili kuepuka ukatili wa kijinsia iliyodumu kwa kipindi cha mwaka 2021/22.
Mkurugenzi Mtendaji kutoka shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI, Yassin Ally akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwalimu akichangia mada.
Mwenyekiti wa Chama cha Waalimu Tanzania (CWT) Mkoa Mwanza, Mwl. Lameki Mahewa (kushoto) akimkabidhi cheti cha pongezi Mkurugenzi Mtendaji shirika la KIVULINI, Yassin Ally (kulia) kutokana na mchango wa shirika hilo kuwajengea uwezo waalimu wanawake ili kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii wanayoishi pamoja na kazini.
Waalimu viongozi kitengo cha wanawake kutoka Wilaya za Mkoa Mwanza wakiwa kwenye hafla ya kufunga programu ya kuwajengea uwezo waalimu wanawake kuepuka vitendo vya ukatili wa kijinsia iliyofanyika jijini Mwanza.
Washiriki wakiwa kwenye hafla hiyo.
Kwaya ya Waalimu Misungwi ikitumbuiza.
Cheti cha pongezi kilichotolewa na waalimu mkoa Mwanza kwenda kwa shirika la KIVULINI.

No comments:

Powered by Blogger.