LIVE STREAM ADS

Header Ads

Sheikh akemea vitendo vya ushoga, ulawiti msikitini

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Sheikh wa Msikiti wa Ijumaa (Masjid Al-Jumaa) jijini Mwanza, Sheikh Hamza Mansoor amekemea vitendo vya ushoga na ulawiti ambavyo zinazidi kuripotiwa katika vyombo vya habari na kuwaonya waumini wa msikiti huo kuzingatia na kufuatilia malezi ya watoto wao.

Sheikh Mansoor aliyasema hayo Disemba 09, 2022 baada ya swala ya adhuhuri ikiwa ni jitihada za viongozi wa dini kushirikiana na viongozi wa Serikali na wadau mbalimbali kupaza sauti kuelimisha na kukemea vitendo hivyo haramu.

Alisema hata maandiko kwenye Quran yamekemea vitendo vya ushoga, ubakaji na ulawiti, pia Mtume Mohammad (S.A.W) naye amekemea na kuwakumbusha waumini wa dini ya kiislamu kuzingatia makemeo hayo ili kutomkwaza Mtume wao.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto la KIVULINI, Yassin Ally aliwahimiza waumini wa dini ya kiislamu kufuatilia malezi ya watoto wao kwani baadhi yao wanapichitia changamoto ya ubakaji, ulawiti na ushoja lakini wazazi na walezi wanashindwa kutambua kwa wakati kutokana na ubize walio nao.

Ally aliwashauri wazazi kutengeneza mazingira rafiki kwa watoto wao ili kuwa huru kufichua vitendo vya ukatili wa kijinsia. "watoto wengi wanatishwa kwamba ukisema nitakuua" alisema Ally wakati akiwajengea uwezo waumini wa Msikiti wa Ijumaa kuhusu malezi bora kwa watoto ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Sheikh wa Msikiti wa Ijumaa (Masjid Al-Jumaa) jijini Mwanza, Sheikh Hamza Mansoor akiwahimiza waumini wa dini ya kiislamu kujiepusha na vitendo vya ushoga na ulawiti na kwamba wahakikishe wanafuatilia malezi ya watoto wao ili kuwakinga na vitendo hivyo haramu.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza baada ya swala ya mchana katika Msikiti wa Ijumaa jijini Mwanza na kutumia fursa hiyo kutoa elimu kwa waumini wa dini ya kiislamu kukemea vitendo vya ushoga na ulawiti katika jamii.
Waumini wa Msikiti wa Ijumaa jijini Mwanza wakifuatilia mada kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally.
Sheikh wa Msikiti wa Ijumaa (Masjid Al-Jumaa) jijini Mwanza, Sheikh Hamza Mansoor (kulia) akiteta jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la KIVULINI, Yassin Ally baada ya kutoa elimu na kukemea vitendo vya ushoga na ulawiti.

No comments:

Powered by Blogger.