LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ushirikishwaji hafifu wa wananchi katika miradi ya masoko Dar es salaam chanzo cha Serikali kupoteza mapato

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com 
Mradi wa soko la kisasa la  kibada lililoko wilaya ya kigamboni ,Dar es salaam
***

Na SELEMAN MAHINYA

Ushiriki wa Wananchi katika maendeleo ni suala linalopewa kipaumbele katika Mataifa mengi Ulimwenguni, Ili Taifa liweze kupiga hatua za kimaendeleo na katika kuhakikisha kwamba maendeleo yanahusisha Jamii na Wananchi kiujumla dhana ushirikishwaji wa wananchi katika miradi mbalimbali ya maendeleo katika maeneo yake.Ushirikishwaji wa wananchi katika ngazi mbalimbali za maendeleo utaboresha zaidi uwasilishaji wa huduma za jamii na utendaji wa kazi katika ngazi hizo.


Kwa mujibu wa ripoti ya mkaguzi wa hesabu za serikali ya mwaka 2021 ilibaini kasoro katika ujenzi wa masoko pamoja na changamoto zinazotokana na ukosefu wa upembuzi yakinifu kabla ya kuanza miradi ya ujenzi wa masoko, mazingira yasiyoridhisha ya utendaji kazi, na usimamizi hafifu wa uendeshaji wa masoko. Kasoro nyingine ni ujenzi wa masoko kuchelewa kukamilika na baadhi ya masoko kukamilika lakini kutotumika kama inaonekana kwenye Jedwali.
Nimetembelea mradi wa soko la Kibada linalopatikana wilaya ya kigamboni mkoa wa Dar es salaam  Mradi huu ulitajwa kuwa utatoa ajira kwa wananchi zaidi ya mia tano kwa wakati mmoja utakuwa na sehemu za kuuzia bidhaa toka shambani, sehemu za kuuza bidhaa zilizochambuliwa, migahawa, maduka ya kawaida, taasisi za kifedha kama Benki pamoja na maduka ya kuuza na kununua fedha na zaidi kutatua kadhia ya masoko bubu ambayo wafanya biashara wanafanya shughuli zao katika maeneo ambayo haruhusiwi mfano ni pembezoni mwa barabara.

Ujenzi soko la Kibada Kigamboni  umeanza tarehe 16/08/2019 na uliotajwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.61za kitanzania. “Tuliambiwa kuwa mpaka mwaka 2021 tungekuwa tumeanza kufanya biashara katika soko hilo” Alisema bi Asha Abdula mfanyabiashara wa mbogamboga eneo la kibada.


Aliongeza “Mwaka 2019 walituambia tutoke barabarani na tuje hapa ili tusubiri kukamilika kwa soko hilo lakini mpaka hivi sasa bado hatujaingia japo soko limekamilika, walisema kuna taratibu za kuingia soko humo lakini ndiyo hivyo zinachukua muda mrefu sana na mwingine walishindwa kuvumilia kubaki hapa  wakarudi barabarani ndiyo maana unaona tupo wachache hapa” alisema bi Asha Abdula mfanyabiashara wa mbogamboga eneo la kibada.


Nimemuuliza mwenyekiti wa wafanyabiashara wadogo wadogo wa kibada Mohamed Mohamed anasema  awali anadai halmashauri iliwaambia wataingia sokoni humo mwezi oktoba  lakini hawakuingia sokoni humo.

Mwezi septemba Mkuu wa wilaya ya kigamboni Fatuma Nyangasa alimuagiza Afisa Biashara wa wilaya hiyo Mohamed Nyasama kuhakikisha anatatua haraka changamoto zinazokwamisha kukamilika kwa soko hilo huku akiongeza kuwa soko hilo ni muhimu kwa wilaya kigamboni nakutaja kuwa wananchi wanatakiwa walitumie ili kuongeza pato la wilaya na mkoa kwa ujumla.
Kwa mujibu wa ripoti ya Mkaguzi mkuu wa hesabu serikali Mkoa wa Dar es salaam una miradi ya masoko matatu ambayo kwa sababu tofauti tofauti bado hajaanza kutumika kama ilivyotarajiwa.

Kwanza ni huu mradi wa soko la kibada lililopo halmashauri ya kigamboni ambapo soko hilo mpaka sasa bado halijanza kutumika kutokana na kuchelewa kukamilika kwa mradi huo uliogharimu kiasi cha fedha cha bilioni 6.61, Huku mradi wa soko la Mbagala kuu lililogharimu kiasi cha fedha billion 1.19 nalo likiwa limekamilika lakini  kwa kiasi kikubwa halitumiki Kwa asilimia 78% lipo wazi ,vibanda 141 kati ya vibanda 180 havitumiki katika sokola la mbagala  kuu.

Mradi wa Soko la Mbagala kuu ambalo limekamilika lakini wafanyabiashara wamegomea kuingia kufanya biashara kutokana kukosekana kwa wateja katika eneo ambalo soko limejengwa.


Na soko la Bombom Kiwalani liligharimu kiasi cha fedha zaid ya billion 0.77 nalo limekamilika kwa zaidi ya miezi 10 lakini hadi sasa halitumiki.


Miradi yote hii ni imetumia jumla ya Bilion 8 za kitanzania hivyo kuchelewesha miradi na kutotumika kwa baadhi ya miradi hii kuna pelekea serikali kupoteza mapato ya ushuru ambayo yangekusanywa katika masoko hayo.



Ripoti hiyo imeweka wazi Kutotumika na kuchelewa kukamilika kwa miradi hiyo kunapelekea usumbufu mkubwa kwa wananchi ambao ni  walengwa wa mradi hiyo ( kwa maana wauzaji na wateja)


Baadhi ya athari zifuatazo zilizotajwa na mhesabu wa hesabu za serikali ni  pamoja na : Masoko yaliyokamilika kutotumika kunapelekea Serikali kupoteza mapato ya ushuru wa masoko. Serikali imekwishapoteza jumla ya Shilingi 16.15 bilioni kwa masoko yaliyokamilika na kutokutumika kama yalivyochambuliwa katika ripoti za Mkaguzi.


“Kwa mfano, kutotumika kwa vibanda 237 kwenye soko la Chuno kwa zaidi ya miezi minne kumepelekea H/M Mtwara Mikindani kupoteza mapato ya zaidi ya Shilingi 32.11 millioni. Kama mapato haya yangekusanywa, ingepatikana asilimia inayopaswa kukusanywa kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya masoko hayo” ilisema ripoti hiyo .


PIli, Kukosa usimamizi mzuri wa uendeshaji wa masoko kumepelekea uchakavu wa miundombinu ya masoko nchini. Ubovu wa miundombinu huathiri wafanyabiashara na wanunuzi kiakili na kiafya, hususani katika kukidhi mahitaji muhimu kwenye masoko.


Ripoti ya mkaguzi wa serikali ilipendekeza kuwepo kwa jitihada za Serikali za kutekeleza mradi wa kuendeleza miji ya kimkakati,  Taasisi isiyoya kiserikali ya WAJIBU  imeshauri Halmashauri zifanye upembuzi yakinifu wa maeneo ambayo masoko yanatakiwa kujengwa na kushirikisha wananchi ili kupunguza hatari ya ujenzi wa masoko Yasiyotumika lakini pia kwa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke ipunguze kodi ya vibanda, na kuweka utaratibu wa kuwa na mikataba ya muda mrefu na mfupi ili wafanyabiashara waweze kumudu gharama za kukodi vibanda hivyo vya biashara.

No comments:

Powered by Blogger.