LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kujamiana mapema kwa watoto wa kike yaweza kuwa ndiyo sababu ya mimba za ujana kuto kuisha?

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Na Bupe Mwakusa, Dar
Mimi nina miaka 18 sasa na mtoto wangu ametimiza mwaka sasa Katika ujauzito wangu sikuona changamoto sana japo nilikuwa nafanya kazi za ndani mpaka mimba ilipofikisha miezi tisa na baada ya hapo nirudi nyumbani Ili nijifingue na baada ya maisha kuwa magumu zaidi niliamua kutafuta Kazi za ndani Ili kukidhi mahitaji ya mwanangu na mtoto akiwa na miezi mitatu hivyo Kazi ninayoifanya inanisaidia kukidhi mahitaji ya mwanangu

Namshauri binti ambaye hajaolewa asizae nje ya ndoa ni kazi sana na inaumiza sanaa haya ni maneno ya binti ambaye hakutaka kutaja Jina lake harakati hizi ikiwa ni baada ya kutekelezwa baada ya kubeba mimba.

Mimba za ujana kama chamgamoto kwa dadaMatokeo ya utafiti wa Afya ya Uzazi na mtoto na viashiria vya Maralia Tanzania 2015-2016 kwa kushirikiana na ofisi ya Takwimu ya Taifa imeeleza swala la uzazi na vigezo vyake unasema kuwa uwezo wa kuzaa unatofautiana kwa makazi na kanda .Wanawake wanao ishi katika maeneo ya vijijini Tanzania Bara kwa wasitani wanazaa watoto 6.0 ikilinganishwa na watoto 3.3 miongoni mwa wanawake wa mjini Tanzania Bara.

Imeonesha kuwa uzazi unatofautiana kulingana na viwango vya elimu na uwezo wa kiuchumi wanawake wasio na elimu wanazaa watoto 3.3 zaidi kuliko wanawake wenye elimu ya sekondari au zaidi (watoto 6.9 dhidi ya watoto 3.6) 2015-2916 TDHS-MIS.
Na Pia katika ukurasa wa nne tafiti hizo zimeonesha kuwa wanawake wa kitanzania huanza kujamiana mwaka mmoja kabla ya wanaume wa Tanzania. Wanawake wenye elimu ya sekondari au zaidi huanza kujamiana zaidi ya miaka mitatu baada ya wanawake wasiyo na elimu (miaka 19.5 dhidi ya miaka 16.5)

Kutokana na hayo ripoti imebainisha kuwa kwa ujumla 27% ya wanawake vijana wenye umri kati ya miaka 15-19 tayari wana watoto au ni wajawazito wa watoto wao wa kwanza.

Wanawake wasio vijana wasio na elimu wana uwezekano wa kuanza kuzaa mara tano zaidi ya wale walio na elimu au zaidi (52% dhidi ya 10%) TDHS-MIS 2015-2016.
Kutokana matokeo ya utafiti huo je ni yapi yaweza tokea endapo mimba za ujana hazitakomeshwa?Yafuatayo ni maoni mbalimbali ya baadhi ya wadau wakieleza swala la mimba za ujana zinavyoweza kuathiri katika nyanja tuu fotauti.

Mtaalamu wa afya Dr Daniel Magomere Kitaalamu umri mzuri wa kuzaa mtoto ni kuanzaia miaka 20 na kuendelea hivyo inapotokea kuwa binti anapata mimba chini ya umri huo au baada ya kuvunja ungo Ameeleza kuwa zipo changamoto nyingi zanazoweza kujitokeza Kwa mama na mtoto na Kwa jamii Kwa mama anaweza kupoteza damu nyingi kwasababu via vyake vya uzazi havijakomaa na njia hazijatanuka Hali inayoweza kupelekea upungufu wa damu au kifo.
Dr Daniel Magomere alieleza kuwa athari nyingine anayoweza kukutana nayo binti aliyezaa Katika umri mdogo ni kuathirika kisaikolojia kutokana na kutokuwa na uimara katika uchumi na kuwaza namna anayoweza kumhudumia mtoto Katika Hali ya ukwasi.

Silvia Sosteness ni mtaalamu wa Saikolojia alieleza kuwa binti mdogo anapopata mimba chini ya umri wa miaka 18 sheria bado inatambua kuwa bado ni mtoto na anastahili kupewa mahitaji yote ya msingi kama haki ya elimu ya kusikilizwa na haki nyinginezo hivyo anapopata mtoto anapokuwa mtoto anaweza kupata msongo wa mawazo na Sonoma. Watoto wanapopata watoto wanapaswa kuthaminiwa ili kuepusha changamoto zinazoweza kuwakabili kama kutengwa na kijiua.
Je kiuchumi inakuwaje?
Mtaalamu wa Uchumi GoodLuck Ningo amesema kuwa Athari za mimba za ujana kiuchumi zipo kwasababu ukiangalia mimba za Ujana zinakuwa ni chini ya miaka 20 hivyo inakuwa bado Mtu hana elimu ya kutosha kulingana na mifumo ya kielimu iliyopo hivyo endapo kama Mtu atakuwa na elimu ya kutosha anaweza kuzalisha zaidi na kuchangia zaidi kwenye uchumi na Pato la Taifa. 

Hivyo kuondoka kabla ya kumaliza elimu inaweza kuathiri uchumi maana Katika umri huo wengi wao wanakuwa bado hawana uwezo wa kujimudu kimaisha.
Bado jamii ina wajibu wa kuhakikisha kuwa watoto wanakuwa salama ili kila mmoja atimize malengo.

No comments:

Powered by Blogger.