LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wizara ya Madini yatoa Tuzo kwa Waandishi wa Habari

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwanahabari George Binagi kutoka BMG akipokea tuzo iliyotolewa na Wizara ya Madini Disemba 17, 2022 jijini Dar es salaam wakati wa Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari, mgeni rasmi akiwa Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye. 
***

Wizara ya Madini imetoa tuzo kwa waandishi wa habari bora kwa upande wa Sekta ya Madini kwenye Kongamano la Maendeleo ya Sekta ya Habari lililofanyika katika ukumbi wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.

Tuzo hizo zimekabidhiwa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye aliyekuwa mgeni rasmi kwa waandishi hao ambapo walipatikana kwa kushirikisha vitengo vya Habari vya Wizara ya Madini na Taasisi zake.

Waandishi waliopata tuzo hizo ni pamoja na Nelly Mtema (Daily News), George Binagi (BMG Media) na Mohammed Zengwa (Global TV).

Kongamano hilo la siku moja linakutanisha wadau wa habari ikiwa ni pamoja na wahariri na wamiliki wa vyombo vya habari, jukwaa la wahariri wa habari, maafisa habari kutoka Serikalini, taasisi binafsi na mashirika ya kimataifa. 

Awali akizungumza katika Kongamano hilo, Waziri Nape amepongeza waandishi wa habari kwa kazi nzuri ya kuelimisha umma na kusisitiza kuwa Serikali itaendelea kushirikiana nao pamoja na kutatua changamoto zinazowakabili.
Na Steven Nyamiti, WM
Mwanahabari Nelly Mtema kutoka Daily News akipokea tuzo.
Mwanahabari Mohamed Zengwa kutoka Global TV akipokea tuzo.
Wanahabari waliopokea tuzo wakiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya Maafisa Habari kutoka Wizara ya Madini.
Tuzo kutoka Wizara ya Madini kutambua mchango wa Waandishi wa Habari katika kuandika na kuripoti habari za Wizara hiyo.

No comments:

Powered by Blogger.