LIVE STREAM ADS

Header Ads

Bilioni 113 kutekeleza miradi ya Meli Ziwa Victoria, Tanganyika

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kampuni ya Huduma za Meli nchini (MSCL) inatarajia kutumia shilingi bilioni 113 katika kipindi cha mwaka wa fedha 2022/23 kutekeleza miradi mbalimbali ya ujenzi wa meli mpya na ukarabati wa meli zilizopo.

Hayo yalibainishwa na Afisa Mahusiano MSCL, Edmond Rutagama wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Mwanza kuhusu utekelezaji wa Miradi ya meli inayoendelea kutekelezwa na kampuni hiyo ikiwemo ujenzi wa meli mpya ya MV. Mwanza "Hapa Kazi Tu".

Rutajama alieleza kuwa miradi saba itakayo gharimu kiasi cha shilingi bilioni 53 itakuwa katika Ziwa Tanganyika na miradi mitano itakayogharimu kiasi cha shilingi bilioni 57 itakuwa ndani ya Ziwa Victoria huku shilingi bilioni mbili zikitumika kuendesha meli zilizopokelewa kutoka Mamlaka ya Bandari nchini (TPA).
Rutajama (katikati) alieleza kuwa meli ya MV. Mwanza "Hapa Hazi Tu" hadi kukamilika itagharimu shilingi bilioni 108 ambapo tayari imefika asilimia 80.

"Meli hii ya MV. Mwanza Hapa Kazi Tu ni kubwa kuliko meli zote katika ukanda wa maziwa makuu, ni meli ambayo imetuheshimisha wananchi na Serikali kwa ujumla" alisema Rutajama.

Pia Rutajama alimshukru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan wa kuendelea kutenga fedha na kuifanya kampuni ya MSCL kuimarika na kuendelea kutekeleza miradi mikubwa ya meli nchini.
Waandishi wa Habari wakinasa matukio.
Na Neema Kandoro, Mwanza

No comments:

Powered by Blogger.