MWANZA: MWAREDDA na UVDS wamaliza tofauti zao
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti wa Umoja wa Madereva Mkoa Mwanza (MWAREDDA), Mjarifu Manyasi (kulia) akibadilishana hati ya makubaliano (MoU) na Mwenyekiti wa Umoja wa Makondakta na Wapiga Debe Mkoa Mwanza (UVDS), Mlimi Juma (kushoto) wakati wa hafla fupi ya muungano wa vyama hivyo iliyofanyika Jumapili Januari 29, 2023 Isamo Hotel jijini Mwanza.
Muungano huo sasa unaondoa mvutano wa muda mrefu uliokuwepo baina ya pande zote mbili kutokana na muingiliano wa kimajukumu ambapo kuanzia sasa viongozi na wanachama wa vyama hivyo wataanza kushirikiana na shughuli mbalimbali.
Viongozi wote wameahidi kushirikiana pamoja na kuondoa na kuzika tofauti za mwingiliano wa majukumu zilizokuwepo hapo awali.
Mwenyekiti wa MWAREDDA, Mjarifu Manyasi (kulia) pamoja na Mwenyekiti wa UVDS, Mlimi Juma (wa pili kushoto) wakionyesha hati ya makubaliano baada ya vyama hivyo kuungana ili kufanya kazi kwa pamoja kwa maslahi ya madereva, makondakta, wapiga debe na abiria.
Mwenyekiti wa MWAREDDA, Mjarifu Manyasi.
Mwenyekiti wa UVDS, Mlimi Juma.
Mwenyekiti wa MWAREDDA, Mjarifu Manyasi akizungumza kwenye hafla hiyo.
Mwenyekiti wa UVDS, Mlimi Juma akizungumza kwenye hafla hiyo.
Katibu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta ya Mawasiliano na Usafirishaji (COTWU- T) Kanda ya Ziwa, Hamza Yusuph akitoa nasaha kwa wanachama wa MWAREDDA NA UVDS baada ya kuungana kufanya kazi pamoja.
Mlezi wa MWAREDDA na UVDS, Noah Makusanya akitoa nasaha zake.
Wanachama wa MWAREDDA na UVDS wakiwa kwenye hafla fupi ya kusaini makubaliano ya kuungana pamoja.
Picha ya pamoja wanachana na viongozi wa MWAREDDA na UVDS baada ya kuungana na kukubaliana kufanya kazi kwa ushirikiano.
PIA SOMA>>> Habari zaidi hapa
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
No comments: