LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mwenyekiti UWT Taifa atoa maagizo kwa Mkurugenzi Jiji la Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mkurugenzi Mtendaji wa Halamshauri ya Jiji la Mwanza, Yahya Sekiete ametakiwa kuboresha miundombinu ya soko la wakulima na wajasiriamali Mirongo ili kuondoa adha iliyopo katika soko hilo.

Agizo hilo lilitolewa Januari 29, 2023 na Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda ambaye pia ni Mkumbe wa Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi Taifa (MNEC) alipofanya ziara katika soko hilo na kuzungumza na wanawake wajasiriamali ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 46 tangu kuasisiwa kwa CCM.

Chatanda baada ya kukagua soko la Mirongo alibaini baadhi ya wajasiriamali wanafanya shughuli zao katika maeneo ambayo hayana paa na hivyo kupata adha ya jua pamoja na mvua na hivyo kuagiza Halmashauri ya Jiji la Mwanza kuhakikisha inashughulikia changamoto hiyo.

Pia Chatanda alitoa pongezi kwa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI kwa kuonyesha mfano na kujenga mabanda mawili pamoja na kituo cha maelezi ya watoto na akina mama kunyonyeshea ambapo aliunga mkono jitihada hizo kwa kuchangia mifuko 50 ya simenti ili kusaidia maboresho zaidi ya soko hilo.

Naye mmoja wa wajasiriamali wa soko hilo, Amina Khamis alisema soko hilo lina zaidi ya wajasiriamali 900 ambapo nusu yao ndio wamepata nafasi katika mabanda yaliyojengwa na shirika la KIVULIN.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally alisema utafiti uliofanywa na shirika hilo ulibaini wajasiriamali katika soko hilo walikuwa wakipata hasara kati ya shilingi 100,000 hadi 150,000 kwa mwezi kutokana na bidhaa zao hususani za matunda kuharibika wakati wa mvua.

“Tumejenga soko la gharama nafuu, tunashauri kila Halmashauri nchini zikaja na mpango kazi wa kuboresha masoko hata mawili kila mwaka ili kuweka mazingira salama kwa wajasiriamali hususani wanawake kufanya biashara zao na kuinua uchumi wao na Taifa kwa ujumla” alisema Ally.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda akizungumza alipofanya ziara katika soko la Mirongo jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa Mwanza, Witness Makale akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi (kulia) akizungumza kwenye ziara hilo.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akizungumza wakati wa ziara hiyo.
Mmoja wa wajasiriamali soko la Mirongo (kulia), Amina Khamis (kulia) akikabidhi risala kwa Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chayanda (kushoto).
Mifuko 50 ya simenti iliyotolewa na Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda kusaidia maboresho ya soko la Mirongo jijini Mwanza.
Makabidhiano ya mifuko ya simenti kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya soko la Mirongo.
Makabidhiano ya mifuko ya simenti kwa ajili ya kuboresha miundombinu ya soko la Mirongo.
Mapokezi ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda katika soko la Mirongo jijini Mwanza.
Mapokezi ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda katika soko la Mirongo jijini Mwanza.
Mapokezi ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda katika soko la Mirongo jijini Mwanza.
Mkuu wa Wilaya Nyamagana, Amina Makilagi (kushoto) akizungumza wakati wa mapokezi ya Mapokezi ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda katika soko la Mirongo jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda (katikati) alipowasili katika soko la Mirongo jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa Mwanza, Witness Makale akizungumza wakati wa mapokezi ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda.
Mapokezi ya Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda katika soko la Mirongo jijini Mwanza.
Mwonekano wa moja ya paa lililojengwa na shirika la KIVULINI katika soko la Mirongo jijini Mwanza.
Watoto wakicheza katika eneo la kituo cha malezi na makuzi ya watoto kilichojengwa na shirika la KIVULINI katika soko la Mirongo.
Akina mama wajasiriamali wakinyonyesha watoto wao katika jengo la Kituo cha malezi na makuzi ya watoto kilichojengwa na shirika la KIVULINI katika soko la Mirongo.
Mwonekano wa Kituo cha Malezi na Makuzi ya Watoto kilichojengwa katika soko la Mirongo jijini Mwanza. Shirika la Kivulini lilijengwa kituo hicho pamoja na majengo/ paa mawili katika soko hilo kwa gharama ya shilingi milioni 88.

No comments:

Powered by Blogger.