LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mbunge wa Kilolo Justine Nyamoga aendelea kufanya makubwa atoa kompyuta 160 kwa shule 10 jimboni

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kilolo wakionesha furaha yao baada ya kukabidhiwa kompyuta mpakato na Mbunge wa Jimbo la Kilolo, Justine Nyamoga (katikati) ambaye ametoa kompyuta 160 kwenye shule 10 za Sekondari katika jimbo lake. Hafla ya kukabidhi kompyuta hizo imefanyika leo Februari 23, 2023 katika shule hiyo.

Na Mwandishi WetuKilolo, Iringa

KATIKA kuinua kiwango cha elimu, Mbunge wa Kilolo, Justine Nyamoga amegawa kompyuta 160 kwenye shule 10 za Sekondari katika jimbo lake.

Shule za Sekondari zilizopewa kompyuta hizo ni Mlafu, Mtitu, Kilolo, Dabaga, Ilula, Ukwega, Mawambala, Nyanzwa, Makwema na Udekwa.

Nyamoga ametoa kompyuta hizo ili kuwasaidia wanafunzi kwenda sambamba na ukuaji wa sayansi na teknolojia hasa ya habari na mawasiliano.

Kompyuta hizo zinatokana na ushirikiano uliopo baina ya Mbunge Nyamoga, Shirika la Upendo Umoja na wafadhili kutoka nje ya nchi.

“Ilikuwa ukienda Bodi ya Mikopo kuangalia majina ya wanafunzi walioomba wengine unawakosa, kumbe hawakukamilisha kujaza fomu kwenye mtandao kwa sababu hawana uelewa na kompyuta. Hii itawasaidia,” amesema Nyamoga.

Amesema lengo lake ni kuhakikisha shule zote za Sekondari za Jimbo hilo zinapata kompyuta zaidi ya 10, ili wanafunzi waweze kujifunza.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo, Anna Msolla amesema maada huo umekuja wakati muafaka.

“Tunamshukuru Mbunge Nyamoga na tunamuombea kwa Mungu aendelee kufanya kazi nyingi zaidi kwa wananchi, kompyuta hizi ni muhimu sana kwa wanafunzi wetu,” amesema Msolla.

Mmoja wa wanafunzi hao akijaribu kuitumia moja ya kompyuta walizokabidhiwa na mbunge huyo.

 Mbunge wa Kilolo, Justine Nyamoga akizungumza na wanafunzi wa sekondari hiyo baada ya kuwakabidhi kompyuta hizo.

Hafla ya utoaji wa kompyuta hizo ikiendelea.

  Mbunge wa Kilolo, Justine Nyamoga (katikati) akikabidhi kompyuta hizo kwa wanafunzi wa Sekondari ya Kilolo kwa niaba ya wanafunzi wa shule hizo 10 ambao waliwakilishwa na walimu wao.

No comments:

Powered by Blogger.