LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wadau wahimizwa kutekeleza kwa vitendo Mwongozo wa kutokomeza Ukatili wa Kijinsia

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Katika kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinatokomezwa katika jamii, Serikali imekuja na mwongozo maalum utakaosaidia kukabiliana na vitendo hivyo katika maeneo ya umma hususani katika masoko.

Kaimu Mkurugenzi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Rennie Gondwe amesema utekelezaji wa mpango huo utaanzia katika masoko ambako vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo wa kisaikolojia na kiuchumi vimeshamiri.

Gondwe ameyasema hayo Februari 27, 2023 jijini Mwanza wakati wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mwongozo huo wa kukabiliana na vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma kilichowashirikisha wadau mbalimbali kutoka Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Geita na Shinyanga.

Amesema wadau hao ambao ni pamoja na maafisa biashara, maendeleo ya jamii, ustawi, viongozi wa masoko na machinga watajadili namna bora ya kutekeleza mwongozo huo ambao pia unaelekeza kuanzishwa kwa madawati ya kushughulikia changamoto za kijinsia na vituo vya malezi/ kunyonyeshea watoto katika masoko nchini.

Awali akifungua kikao kazi hicho, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya amewahimiza wadau hao kujadili na kuweka mikakati itakayosaidia utekelezaji wa mpango huo kwa vitendo ili kukabiliana na changamoto za ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma hususani katika masoko.

Balandya amesema Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kufanya kazi kubwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kutatua changamoto za wananchi na kuhakikisha kila mtu anafanya shughuli zake kwa uhuru, amani na bila kudhalilishwa.

Nao baadhi ya washiriki wa kikao kazi hicho akiwemo Afisa Maendeleo Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela, Sarah Nthangu pamoja na Afisa Biashara Halmashauri ya Wilaya ya Ukerewe, John Kilunge wamesema mwongozo huo utasaidia kuwalinda wanawake na watoto ambao ni wahanga wakubwa wa vitendo vya ukatili wa kijinsia katika jamii/ maeneo ya umma hususani katika masoko.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya akifungua kikao kazi kilichowashirikisha wadau wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwemo Maafisa Biashara, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Viongozi wa Machinga na Masoko kutoka mikoa ya Mwanza, Geita na Shinyanga chenye lengo la kujadili utekelezaji wa mwongozo wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma hususani masoko.
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya akifungua kikao cha wadau wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia chenye lengo la kujadili utekelezaji wa mwongozo wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Jinsia kutoka Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Rennie Gondwe (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu utekelezaji wa mwongozo wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma hususani masokoni.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii kutoka Halmashauri za mikoa ya Mwanza, Geita na Shinyanga wakiwa kwenye kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mwongozo wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma.
Wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa masoko wakiwa kwenye kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mwongozo wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma.
Wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa machinga wakiwa kwenye kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mwongozo wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma.
Wadau mbalimbali wakiwemo Maafisa Biashara, Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Viongozi wa Machinga na Masoko wakiwa kwenye kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mwongozo wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma ambao utekelezaji wake unaanza na masokoni.
Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mwongozo wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma ikiwemo masoko.
Mgeni rasmi, Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Elikana Balandya akiwa kwenye picha ya pamoja na washiriki wa kikao kazi cha kujadili utekelezaji wa mwongozo wa kuzuia vitendo vya ukatili wa kijinsia katika maeneo ya umma kilichofanyika jijini Mwanza.

No comments:

Powered by Blogger.