LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi Mwanza wapewa tahadhari kujikinga na ugonjwa wa Marburg

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com jikinge-na-marburg
Wananchi mkoani Mwanza wametakiwa kuchukua tafadhari ili kujikinga na maambukizi ya ugonjwa wa homa ya vizuri vya Marburg ambao umeripotia hivi karibuni katika Mkoa jirani wa Kagera.

Mganga Mkuu Mkoa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachunzibwa ametoa rai hiyo Machi 24, 2023 wakati wa kikao cha kuelimisha wadau mbalimbali wakiwemo viongozi wa dini, afya, wavuvi, machinga, masoko, NGO's na makundi ya kijamii kuhusu ugonjwa huo.

Amesema licha ya kwamba ugonjwa huo haujaripotiwa kuingitia mkoani Mwanza, lakini bado wananchi wanapaswa kuchukua tahadhari za kujikinga ikiwemo kuepuka misongamano, kuzingatia usafi, kunawa mikono kwa majitiririka na kuzingatia matumizi ya vitakasa mikono.

Dkt. Rutachunzibwa amewataka wadau walioshiriki kikao hicho kwenda kuwaelimisha wananchi kuhusu ili kutambua dalili za ugonjwa huo wa homa ya Marburg na jinsi ya kujikinga.

Akitoa wasilisho kuhusu ugonjwa huo, Mratibu wa Elimu ya Afya mkoani Mwanza, Renard Mlyakado amesema wananchi wanapaswa kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya wanapoona mgonjwa ana dalili za awali ambazo ni homa kali, mwili kuishiwa nguvu, maumivu makali ya kichwa na misuli, macho kuwa mekundu, kuwa na vidonda vya koo, vipele vya ngozi na maumivu ya tumbo.

Mlyakado amebainisha kuwa dalili za baadae ni pamoja na kutapika na kuhara damu, kutoka damu puani na kutokwa jasho ambapo amewataharadhisha wananchi kuepuka kugusana na mgonjwa mwenye dalili hizo ama kutumia vifaa alivyotumia ikiwemo mavazi na kwamba wanapaswa kutoa taarifa kwa wataalamu wa afya.

Naye Katibu Tawala Msaidizi Mkoa Mwanza, Chagu Ng'oma amesema Mkoa unaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa huo kwa kutoa elimu kwa makundi mbalimbali wakiwemo wavuvi ambayo yana mwingiliano mkubwa wa watu ili kuhakikisha ugonjwa huo hauingii mkoani Mwanza.

Washiriki wa kikao hicho wakiwemo viongozi wa dini na wavuvi wameahidi kutumia majukwaa yao kuelimisha jamii ili kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya ugonjwa wa Marburg ambao bado hauna tiba wala chanjo ambapo mgonjwa hutibiwa kulingana na dalili alizonazo.

Itakumbukwa Machi 16, 2023 Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt. Tumaini Nagu alitoa taarifa ya kuibuka ugonjwa usiojulikana mkoani Kagera ambao ulisababisha vifo vya watu watano kati ya wanane waliobainika ambapo hadi sasa jumla ya washukiwa 193 wako kwenye uangalizi maalum.

Baadae Machi 21, 2023 Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu aliweka wazi kwamba ugonjwa huo ulikuwa ni homa ya Marburg ambao maambukizi yake huanzia kwa wanyama kama popo, tumbili, nyani na swala wa porini na hivyo wananchi kutahadharishwa kutochangamana ama kula kitoweo cha wanyama hao.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mganga Mkuu Mkoa Mwanza, Dkt. Thomas Rutachunzibwa akizungumza wakati wa kikao cha wadau mbalimbali mkoani Mwanza kilicholenga kutoa elimu kuhusu mlipuko wa ugonjwa wa Marburg.
Mchungaji Elihuruma Swai wa Kanisa TAG Nazareth jijini Mwanza akichangia afua mbalimbali za kuchukuliwa ili kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Marburg.
Viongozi wa dini pia wamekubaliana kutumia majukwaa yao kutoa elimu kwa jamii kujikinga na maambukizi ya virusi vya Marburg.
Msemaji wa Chama cha Wavuvi Tanzania, Sijaona James akieleza utayari wa chama hicho kuwafikia wavuvi katika mialo mbalimbali mkoani Mwanza kwa ajili ya kutoa elimu ya kukabiliana na maambukizi ya virusi vya Marburg.
Viongozi mbalimbali wakiwemo wa dini wakiwa kwenye kikao hicho.

No comments:

Powered by Blogger.