LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kiwanda cha Wanawake Sengerema chakabiliwa na uhaba wa maziwa

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kikundi cha Wanawake Kahumulo kilichopo Wilaya ya Sengerema mkoani Mwanza kinachoendesha mradi wa kiwanda kidogo cha kuchakata maziwa kimeomba kuwezeshwa ng’ombe ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa maziwa.

Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango na Fedha ya kikundi hicho, Elizabert Michael amesema wanakumbana na changamoto ya upatikanaji wa maziwa kutoka kwa wafugaji hivyo wakijikita kwenye ufugaji wataondokana na changamoto hiyo.

Naye Mkurugenzi wa shirika la Mikono Yetu, Maimuna Kanyama amesema shirika hilo liliwajengea uwezo wanawake hao na kufanikiwa kuanzishwa miradi mbalimbali ikiwemo kiwanda hicho ambacho hadi sasa kimegharimu shilingi milioni 30 na kwamba hadi kukamilika kitagharimu milioni 50.

Kanyamala amesema kiwanda hicho kimetoa fursa kwa wanawake 128 hivyo ni vyema Serikali ikawaunga mkono kwa kusaidia utatuzi wa changamoto zinazowakabili ikiwemo kuwafikishia huduma ya umeme na maji.

Hayo yalijiri wakati wa zoezi la upandaji migomba katika mazingira ya kiwanda hicho lililoambatana na kuwajengea uwezo wanawake kujikwamua kiuchumi ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya siku ya wanawake duniani iliyoadhimishwa na shirika la Mikono Yetu katika Kijiji cha Kahumulo Machi, 08, 2023.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Mikono Yetu la jijini Mwanza, Maimuna Kanyamala (kushoto) akishuhudia zoezi la upandaji migomba katika mazingira ya kiwanda cha kuchakata maziwa Kahumulo wilayani Sengerema.
Meneja wa SIDO Mkoa Mwanza, Bakari Songwe (kulia) ambaye ni mlezi wa kikundi cha wanawake Kahumulo akishuhudia zoezi la upandaji migomba katika kiwanda cha kuchakata maziwa.
Wanawake kikundi cha Kahumulo wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Mkurugenzi wa shirika la Mikono Yetu, Maimuna Kanyama (mwenye miwani) akiwa kwenye picha ya pamoja na wanawake kikundi cha Kahumulo wilayani Sengerema.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.