LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wateja wa CRDB kujishindia simu, magari na fedha milioni 350

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Benki ya CRDB imetenga zawadi mbalimbali ikiwemo simu janja pamoja na magari kwa ajili ya watumiaji wa huduma ya SimBanking ambayo inarahisha upatikanaji wa huduma mahali popote na kuondoa msongamano katika matawi ya benki hiyo.

Hayo yamebainishwa na Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Jeremiah Msemo wakati akizungumzia kampeni ya Benki ni SimBanking kupitia kituo cha redio cha Radio Free Africa (RFA) na kubainisha kuwa simu zaidi ya 200, magari sita na fedha shilingi milioni 350.

Naye Meneja wa CRDB Tawi la Nyerere jijini Mwanza, Godlove Marwa amesema kampeni hiyo ilizinduliwa mwezi Feberuari mwaka huu ambapo aliwahimiza wateja wa benki hiyo kutumia huduma ya SimBanking kufanya miamala mbalimbali ili kupata fursa ya kujishindia zawadi hizo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Viongozi wa benki ya CRDB wakiwa katika kituo cha matangazo ya redio RFA kutoa elimu kwa wateja kuhusiana na huduma mbalimbali ikiwemo SimBanking.
Viongozi wa benki ya CRDB wakiwa kwenye mahojiano RFA.
Viongozi wa CRDB wakiteta jambo.
Viongozi wengine wa CRDB walioshiriki kwenye hamasa ya kampeni ya Benki ni SimBanking jijini Mwanza ni Meneja tawi la Rock City- Jesca Kikoito, Meneja Biashara tawi la SAUT- Shaban Mama, Meneja Mahusiano Huduma Mbadala za Kibenki Kanda ya Ziwa- Erasto Magoto, Meneja Tawi la Nyerere- Medard Kayombo, Afisa Mikopo tawi la Mwanza- Huduma Gadiel, Meneja Mahusiano Mikopo ya Kilimo Kanda ya Ziwa- Michael Jacob, Afisa Mikopo tawi la Nyerere- Pendo Ndeki na Wakili wa CRDB Kanda ya Ziwa- Irene Baisi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.