LIVE STREAM ADS

Header Ads

Jumuiya ya LVRLAC kupanda miti milioni moja wilayani Ilemela

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mwenyekiti wa LVRLAC Kanda ya Tanzania, William Gumbo akiongoza zoezi la upandani miti katika Kituo cha Afya Karume wilayani Ilemela.
***

Jumuiya ya Serikali za Mitaa (LVRLAC) Kanda ya Tanzania kwa kushirikiana na benki ya DTB inatarajia kupanda miche milioni moja katika Wilaya ya Ilemela mkoani Mwanza ikiwa ni jitihada za kuhamasisha utunzaji mazingira katika jamii.

Hayo yamebainishwa Machi 29, 2023 na Katibu Mkuu wa Jumuiya hiyo, Billy Brown wakati wa zoezi la kufanya usafi katika fukwe ya Igombe na kupanda miti katika Kituo cha Afya Karume wilayani Ilemela, kuelekea mkutano wa 27 wa LVRLAC Machi 30-31, 2023 ukumbi wa Rock City.

Brown amesema jumuiya hiyo kwa kushirikiana na wadau mbalimbali inaendelea kuhamasisha jamii kutunza mazingira kwa kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi pamoja na kuimarisha usalama wa Ziwa Victoria kwa manufaa ya wananchi na mataifa yanayozunguka ziwa hilo.

Jumuiya ya LVRLAC inaundwa na Halmashauri zinazozunguka Ziwa Victoria katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ambapo kwa Tanzania, Halmashauri hizo zinapatikana mikoa ya Kanda ya Ziwa.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Katibu wa LVRLAC, Billy Brown (kushoto) na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela (kulia) wakipanda mti katika Kituo cha Afya Karume.


Mwenyekiti wa LVRLAC Kanda ya Tanzania ambaye pia ni Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Musoma, William Gumbo akiwahimiza wananchi kuimarisha usafi katika fukwe za Ziwa Victoria pamoja na kuwa na utamaduni wa kupanda miti.
Katibu Mkuu LVRLAC Kanda ya Tanzania, Billy Brouwn akizungumza wakati wa zoezi la kufanya usafi na kupanda miti katika eneo la Igombe wilayani Ilemela.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.