LIVE STREAM ADS

Header Ads

Mratibu taasisi ya TOMA akutana na wanahabari mkoani Shinyanga

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Mratibu wa taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni (Tanzania Online Media Alliance- TOMA) Seif Mangwangi amekutana na kuzungumza na baadhi ya waandishi wa habari za mtandaoni Mkoa wa Shinyanga.

Kikao hicho kimefanyika Machi 27, 2023 ambapo pamoja na mambo mengine Mkurugenzi Mangwangi ameelezea faida za waandishi wa habari hao kujiunga na Taasisi ta TOMA katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku.

Mangwangi ametumia nafasi hiyo pia kuelezea majukumu ya TOMA katika Tasnia ya habari huku akihamasisha waandishi hao kujiunga na taasisi ya waandishi wa habari mtandaoni (TOMA) ambayo inapokea waandishi wote wenye utayari hapa Nchini.

Taasisi ya TOMA inasimamia vyombo mbalimbali vya habari ikiwemo Blogs na Online Tv katika mikoa mbalimbali nchini Tanzania kwa kutatua kero na changamoto ikiwa ni pamoja na kutoa fursa mbalimbali kwa waandishi wa habari za mtandaoni.
Mratibu wa TOMA akizungumza na wanahabari mkoani Shinyanga. Mratibu wa TOMA akizungumza akizungumza na wanahabari wa mtandaoni mkoani Shinyanga. Mratibu wa TOMA Seif akizungumza kwenye kikao cha pamoja na baadhi waandishi wa habari za mtandaoni Mkoa wa Shinyanga.
Mratibu wa TOMA akizungumza kwenye kikao cha pamoja na baadhi waandishi wa habari za mtandaoni Mkoa wa Shinyanga
Mratibu wa TOMA akizungumza na wanahabari mkoani Shinyanga.
Baadhi ya waandishi wa habari za mtandaoni Mkoa wa Shinyanga wakiwa katika kikao cha pamoja na Mratibu wa TOMA.
Mratibu wa Shinyanga Press Club (kushoto) Estomain Henry akiwa na Mratibu wa TOMA, Seif Mangwagi (kulia).
Mratibu wa Shinyanga Press Club (kushoto) Estomain Henry akiwa na Mratibu wa TOMA, Seif Mangwagi (kulia).
Upande wa kushoto ni Mratibu wa Shinyanga Press Club, Estomain Henry akiuliza maswali kwa Mratibu wa TOMA, Seif Mangwagi.
Mratibu wa TOMA, Seif Mangwagi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari za mtandaoni Mkoa wa Shinyanga.

Mratibu wa TOMA, Seif Mangwagi akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya waandishi wa habari za mtandaoni mkoani Shinyanga.
Na Mapuli Misalaba, Shinyanga

No comments:

Powered by Blogger.