LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais wa Zanziba, Mstaafu Kikwete watunukiwa Tuzo

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi na Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete ni miongoni mwa Viongozi Sita waliokabidhiwa Tuzo ya Rais (Presidential Award) ya Mwaka 2023 inayotolewa na Taasisi ya Global Water Changemakers.

Tuzo hiyo imetolewa kwa mara ya kwanza mwaka huu kwa Wakuu wa Nchi na Serikali 6 waliopo madarakani na waliostaafu kwa kutambua mchango wao katika kuonesha dhamira ya kweli ya kusimamia na kuleta mabadiliko chanya katika kuendeleza sekta ya maji katika nchi wanazotoka na barani Afrika.

Tuzo hizo zimekabidhiwa na Mhe. Mokgweetsi Masisi, Rais wa Botswana katika Kongamano la Umoja wa Mataifa kuhusu Maji linaloendelea jijini New York, Marekani Machi 22, 2023.

Viongozi waliopokea tuzo hizo ni Wenyeviti wenza wanne wa Jopo la Ngazi ya Juu la Kimataifa la Uwekezaji wa Maji kwa Afrika ambao ni Rais Macky Sall wa Senegal, Rais Hage Geingob wa Namibia, Waziri Mkuu wa Uholanzi, Mark Rutte na Rais Mstaafu Dkt. Jakaya Kikwete wa Tanzania.
Na Mwandishi Maalum

No comments:

Powered by Blogger.