MSD YAANDAA SEMINA KWA WAHARIRI VYOMBO VYA HABARI

Na Dotto Mwaibale, Babati
Bohari ya Dawa (MSD) imeandaa Semina maalum kwa
Wahariri wa vyombo vya habari nchini itakayofanyika kwa siku mbili mkoani
Dodoma.
Katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi Mkuu wa
MSD, Mavere Tukai imeeleza kuwa semina hiyo itaanza kesho Aprili 05, 2023 na
kufikia tamati kesho kutwa Aprili 06, 2023 na kuwa itafanyika katika ukumbi wa
Tume ya Uchaguzi mkoani humo.
"Lengo la semina hii ni kuwajengea uelewa
kuhusu majukumu ya MSD ambayo ni manne ya kuzalisha, kununua, kutunza na
kusambaza bidhaa za afya nchini sambamba na maboresho mbalimbali yanayofanywa
na taasisi hiyo kupitia mpangomkakati wake wa muda mfupi na mrefu" amesema
Tukai.
Tukai amesema mbali na kuwajengea uelewa Wahariri juu ya majukumu na maboresho ya MSD, semina hiyo pia itatoa fursa kwa MSD kutoa ufafanuzi juu ya masuala kadhaa ambayo yamekuwa yakijitokeza kwenye jamii, kufanya ziara naokwenye maghala ya MSD kuangalia mfumo mzima wa mnyororo wa ugavi unavyofanya kazi na kisha kutembelea baadhi ya wateja wa MSD.
No comments: