LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kesi za wanafunzi kupewa ujauzito zapungua wilayani Magu

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shirika la Maendeleo ya Wanawake (Forum for Women and Development- FOKUS) la nchini Norway l limeridhishwa na jitihada mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali kwa kushirikiana na wadau wa maendeleo katika kupambana na kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Hayo yameelezwa Mei 10, 2023 na Mshauri wa Programu ya kuwawezesha wanawake kutoka shirika, Joar Svanemyr wakati wa kikao cha kutoa mrejesho wa mbinu na hatua mbalimbali zinazochukuliwa katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia hususani kwa watoto na wanawake katika Wilaya ya Magu mkoani Mwanza.

Svanemyr amesema shirika hilo litaendelea kufadhili shughuli mbalimbali zinazofanywa na shirika la KIVULINI ambalo linatekeleza mradi wa kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia katika Kata nne kati ya 25 za Wilaya ya Magu ili kuzifikia Kata nyingi zaidi.

Naye Mkurugenzi Mtendaji shirika la KIVULINI, Yassin Ally amesema shirika hilo limetoa elimu kwa wanaharakati ngazi ya jamii zaidi ya 80 ambao wanapita nyumba kwa nyumba kuelimisha jamii katika Kata nne za Sukuma, Jinjimili, Kabila na Nyang’hanga ambazo shirika hilo linatekeleza mradi wa kutokomeza vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Kwa upande wake Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Lilian Michael amesema jamii imekuwa na mwamko wa kuripoti matukio ya vitendo vya ukatili wa kijinsia baada ya kupata elimu ambapo hatua za kisheria zinazochukuliwa zimesaidia kupunguza vitendo vya ukatili wa kijinsia ikiwemo ubakaji, ulawiti, mimba na ndoa za utotoni kwa wanafunzi.

Mkuu wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi wilayani Magu, Bahati Salvatory amesema awali kulikuwa na idadi kubwa ya matukio wanafunzi wa kike kupewa mimba lakini kutokana na elimu iliyotolewa kwa jamii, matukio hayo yamepungua kutoka 111 mwaka 2020 hadi 67 mwaka 2022.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la kutetea haki za wasichana na wanawake KIVULINI, Yassin Ally (kushoto) akizungumza wakati wa kikao cha kutoa mrejesho wa namna viongozi mbalimbali wanashiriki kwenye mapambano dhidi ya vitendo vya ukatili wa kijinsia. 
Waliokaa ni Mshauri wa Programu Shirika la Maendeleo ya Wanawake (Forum for Women and Development- FOKUS) la nchini Norway l, Joar Svanemyr (katikati) na Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Lilian Michael (kulia).
Mshauri wa Programu Shirika la Maendeleo ya Wanawake (Forum for Women and Development- FOKUS) la nchini Norway l, Joar Svanemyr akizungumza kwenye kikao hicho.
Kaimu Afisa Maendeleo ya Jamii Mkoa wa Mwanza, Sarah Nthangu (kulia) akitoa taarifa ya MTAKUWWA wakati wa kikao cha wadau wa kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kilichofanyika wilayani Magu kikiandaliwa na shirika la KIVULINI.
Afisa Maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Wilaya ya Magu, Lilian Michael akitoa taarifa ya vitendo vya ukatili wa kijinsia wilayani humo wakati wa kikao hicho.
Kaimu Mkuu wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Kagemulo Muhula akitoa takwimu za matukio ya ukatili wa kijinsia na hatua zilizochukuliwa wakati wa kikao hicho.
Mkuu wa Dawati la Jinsia kutoka Jeshi la Polisi Wilaya ya Magu, Bahati Salvatory (katikati) akitoa takwimu za matukio ya ukatili wa kijinsia yaliyoripotiwa wilayani humo.
Mkuu wa Shule ya Sekondari Sukuma wilayani Magu, Mwl. Thomas Paul akichangia hoja kwenye kikao hicho.
Wadau mbalimbali wa masuala ya ukatili wa kijinsia ikiwemo jeshi la polisi, waalimu, watendaji na maafisa maendeleo ya jamii wakiwa kwenye kikao hicho.
Picha ya pamoja baada ya kikao hicho.

No comments:

Powered by Blogger.