LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ni uzinduzi wa kishindo 'Transec Lake Victoria Marathon 2023' Mwanza

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Shindano la riadha la "Transec Lake Victoria Marathon 2023" limezinduliwa rasmi kwa kishindo katika fukwe ya Ziwa Victoria jijini Mwanza ambapo zaidi ya wanariadha elfu moja kutoka ndani na nje ya Tanzania wanatarajiwa kushiriki. 

Uzinduzi huo ulifanyika Ijumaa Mei 26, 2023 katika fukwe ya Yatch Club ukiongozwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa ambaye alizindua pia zoezi la usajili kwa kuwa mshiriki wa kwanza kujisajili.

Itakumbukwa mbio ya Transic Lake Victoria Marathon ambayo mwaka huu ni msimu wa tatu mfululizo kufanyika jijini Mwanza, imelenga kuhamasisha utalii wa ndani, uhifadhi wa Ziwa Victoria pamoja na kusaidia makundi yenye uhitaji ikiwemo watoto ambapo uzinduzi huo ulivuta hisia za watu mbalimbali waliohudhuria baada ya kupata fursa ya kutalii ziwani kwa kutumia boti ya kisasa.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Karungwa alisema pamoja na kwamba mbio ya Transec Lake Victoria Marathon inaimarisha afya kwa washiriki lakini pia ina mchango mkubwa kwani fedha zinazopatikana zinarudi kusaidia jamii na hivyo kuimarisha upendo, undugu na burudani ambapo aliwasihi washiriki kujisajili mapema huku pia akiwahimiza wadhamini kujitokeza zaidi kufadhili mbio hiyo.

Naye Mwandaaji wa mbio hiyo ya Transec Lake Victoria Marathon, Rogatus Kabyemera alisema inatarajiwa kufanyika Jumapili Julai 02, 2023 katika viunga vya Jiji la Mwanza na kwamba maandalazi yanaendelea vizuri.

Kwa upande wake Mratibu wa mbio hiyo, Halima Chake aliwashukuru wadhamini wote wakiongozwa na mdhamini mkuu kampuni ya Transec kwa kutoa udhamini msimu wa tatu mfululizo mwaka huu. Aliwataja wadhamini wengine kuwa ni TBL, TDL, NSSF na Rock City Runners.

"Kupitia mbio hiii, mwaka jana tulifanikiwa kuwalipia bima ya matibabu watoto 85 kutoka Kituo cha Watoto Africa kilichopo wilayani Ilemela ambapo mwaka huu tunatarajia kuchangia gharama za matibabu kwa watoto wanaopata matibabu ya saratani katika Hospitali ya Bugando.

Halima alisema gharama za ushiriki zinafanyika kwa njia ya Tigo Lipa Nambari 88 38 49 ambapo Kilomita 2.5 maalumu kwa watoto chini ya miaka 10 ni shilingi 20,000 na mbio za watu wazima kuanzia Kilomita 10 hadi Kilomita 21 ni shilingi 35,000.

Mwakilishi wa kampuni ya Transec inayohusika na biashara ya uagizaji wa vifaa mbalimbali vinavyotumika viwandani na migodini, Victor Okeyo alitoa hamasa kwa wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ikiwemo kushiriki riadha ili kuimarisha afya zao ambapo alitoa hamasa washiriki kujisajili kwa wingi ili kukimbia pamoja kwenye mbio ya Transec Lake Victoria Marathon 2023.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza anayeshughulikia Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Patrick Karangwa akizungumza kwenye uzinduzi wa mbio ya Transec Lake Victoria Marathon inayotarajiwa kufanyika Jumapili Julai 02, 2023 jijini Mwanza.
Mwandaani wa mbio ya Transec Lake Victoria Marathon, Rogatus Kabyemera akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwandaani wa mbio ya Transec Lake Victoria Marathon, Rogatus Kabyemera akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mratibu wa Transec Lake Victoria Marathon akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Programu Meneja kutoka Kituo cha Watoto Africa, Peter Onyango akitoa salamu kwenye uzinduzi huo. Pembeni yake ni Matroni wa Kituo hicho, Tabitha Martin.
Mwakilishi kampuni ya TBL Group, Genes Focus akitoa salamu za TBL na TDL ambao wamedhamini mbio ya Transec Lake Victoria Marathon 2023.
Meneja Mkakati kampuni ya Transec, Victor Okeyo akieleza nia ya kampuni hiyo kujitokeza kudhamini mbio ya Transec Lake Victoria Marathon kuwa ni pamoja na kurejesha fadhila kwa jamii.
Katibu Chama cha Riadha Mkoa Mwanza, Kurwijila Malima akitoa salamu zake wakati wa uzinduzi wa mbio ya Transec Lake Victoria Marathon 2023.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (wa pili kulia) akifungua boksi lenye vifaa mbalimbali ikiwemo jezi itakayotumika wakati wa riadha hiyo ikiwa ni sehemu ya uzinduzi huo.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (katikati) akifungua boksi lenye vifaa mbalimbali ikiwemo jezi itakayotumika wakati wa riadha hiyo.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (katikati) akionyesha nambari ya ushiriki wa mbio ya Transec Lake Victoria Marathon 2023.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (kulia) akipokea jezi rasmi itakayotumika kwenye mbio ya Transec Lake Victoria Marathon 2023 kutoka kwa Mwakilishi wa kampuni ya Transec, Victor Okeyo (kushoto).
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (kulia) akijisajili kushiriki mbio ya Transec Lake Victoria Marathon 2023.
Mratibu wa Transec Lake Victoria Marathon, Halima Chake (wa pili kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi kutoka kampuni ya Transec.
Wadau mbalimbali wakiwa kwenye picha ya pamoja.
Waandishi wa habari za michezo jijini Mwanza nao wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (wa tatu kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadhamini mbalimbali wa Transec Lake Victoria Marathon 2023.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (wa pili kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi kutoka kampuni ya Transec.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi kutoka kampuni ya TBL Group.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanariadha mbalimbali jijini Mwanza.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanariadha mbalimbali jijini Mwanza.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali wa Transec Lake Victoria Marathon 2023.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na MC Magoma (kushoto).
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanariadha mbalimbali jijini Mwanza.
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa akiwa kwenye picha ya pamoja na wanariadha mbalimbali jijini Mwanza.
Utalii wa ndani katika fukwe ya Ziwa Victoria inapotengenezwa meli kubwa na ya kisasa MV- Mwanza "Hapa Kazi Tu".
Mgeni rasmi, Kaimu Katibu Tawala Mkoa Mwanza, Patrick Karungwa (katikati) akibarizi upepo ndani ya Ziwa Victoria na wadau mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Transec Lake Victoria Marathon 2023.
Uzinduzi wa Transec Lake Victoria Marathon uliambatana na burudani ndani ya boti kuzunguka fukwe za Ziwa Victoria ikiwa ni sehemu ya kuhamasisha utalii na uhifadhi wa Ziwa Victoria.
Ikiwa ungependa kushiriki mbio ya Transec Lake Victoria Marathon, Jumapili Julai 02, 2023, piga simu nambari 0758 16 90 40.
Tazama BMG TV hapa chini
PIA SOMA>>> Habari zaidi hapa

No comments:

Powered by Blogger.