LIVE STREAM ADS

Header Ads

Watumishi Misungwi watakiwa kukaa kwenye Vituo vyao vya Kazi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Watumishi wakiwemo waalimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza wametakiwa kukaa/ kuishi katika vituo vyao vya kazi tofauti na ilivyo hivi sasa ambapo baadhi yao wanakaa wilayani nyingine ikiwemo Nyamagana.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya hiyo, Benson Mihayo aliyasema hayo Mei 12, 2023 kwenye mkutano wa wadau wa elimu ulicholenga kutathimini mafanikio na changamoto za elimu wilayani Misungwi pamoja na kukabidhi zawadi kwa waalimu na shule zilizofanya vizuri katika mitihani ya kitaifa ya mwaka 2022.

Mihayo alisema waalimu wanaokaa nje ya vituo vyao vya kazi hawawezi kujua changamoto za mazingira ambayo wanafunzi wanatoka hivyo hawawezi kuwasaidia kwa weledi huku pia wakitumia muda na gharama kufika katika vituo vyao vya kazi akitolea mfano waalimu wanaoishi Kata ya Buhongwa jijini Mwanza huku vituo vyao vya kazi vikiwa Misungwi.

Katika hatua nyingine Mihayo aliwatahadharisha waalimu kupunguza tabia ya kukopa kupita kiasi hatua ambayo inawadhalilisha kwani wanakopa bila sababu za msingi hadi wanamaliza mishahara yao ya mwezi husika akitolea mfano mmoja wa waalimu ambaye alibakiza elfu 50 huku wengine wakisalimisha hadi kadi zao ba benki.

Kutokana na changamoto hiyo ya mikopo kwa waalimu, Mkuu wa Wilaya ya Misungwi Paul Chacha aliwashauri waalimu kutumia muda wao wa ziada kufanya shughuli zinazowaongezea kipato ikiwemo ujasiriamali, biashara na kilimo hatua ambayo itawafanya wajiimarishe kiuchumi na kutimiza majukumu ya mwajiri kwa ufanisi zaidi.

Naye Afisa Elimu Sekondari wilayani Misungwi, Diana Kuboja alisema mikutano ya wadau wa elimu ambayo imekuwa ikifanyika wilayani humo imekuwa chachu ya kuongeza ufaulu kwa wanafunzi kutokana na utekelezaji wa maazimio yanayowekwa kwenye mikutano hiyo, utoaji wa zawadi mbalimbali ikiwemo fedha taslimu na vyeti kwa waalimu na shule zinazofanya vizuri pamoja na zawadi hasi za karipio na vinyago kwa shule zinazofanya vibaya.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkuu wa Wilaya Misungwi, Paul Chacha akizungumza kwenye kikao cha wadau wa elimu wilayani huo ambapo aliwasihi waalimu kufanya kazi kwa uadilifu ili kuboresha ili kuongeza ufaulu kwa wanafunzi.
Mkurugenzi Mtendaji Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi, Benson Mihayo akizungumza kwenye kikao hicho ambapo pia alihimiza wazazi kushirikiana na waalimu kutekeleza mpango wa utoaji chakula kwa wanafunzi.
Afisa Elimu Sekondari wilayani Misungwi, Mwl. Diana Kuboja akizungumza kwenye mkutano huo.
Waalimu ambao shule zao zilifanya vizuri kwenye mitihani ya kitaifa ya darasa la saba na kidato cha nne wakipokea zawadi.
Mkuu wa Wilaya ya Misungwi, Paul Chacha (kulia) akikabidhi zawadi ya fedha na cheti kwa mmoja wa waalimu ambae wanafunzi walifaulu vyema katika mitihani ya kitaifa.
Makabidhiano ya kinyago kwa shule zilizofanya vibaya wilayani Misungwi.
Tazama BMG TV hapa chini

No comments:

Powered by Blogger.