LIVE STREAM ADS

Header Ads

Millagro Car Wash Mwanza yatoa semina kwa waraibu wa dawa za kulevya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kampuni ya uoshaji magari ya Millagro Car Wash imetoa mafunzo kwa waraibu wa dawa za kulevya jijini mwanza ili kuwajengea uwezo kujitambua na kujiepusha na changamoto za afya ya uzazi, ukatili wa kijinsia na saikolojia.

Akizungumza Mei 13, 2023 wakati wa mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Millagro Car Wash Esther Morris ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika la Naweza Tena linalowasaidia waathirika wa dawa za kulevya amesema mafunzo hayo yametolewa kwa baadhi ya waraibu ambao wameacha matumizi ya dawa za kulevya wanaopata tiba ya methadone.

“Jamii inawatenga waraibu wa dawa za kulevya wakiwachukulia kama watu wezi na hatarishi hivyo tuliona ni vyema kuanzisha mradi wa kuosha magari (Millagro Car Wash) ili kuwapa fursa ya kufanya kazi na kujipatia kipato kitakachowasaidia kujitegemea kiuchumi baada ya kuacha matumizi ya dawa za kulevya” alisema Morris.

Morris amesema semina hiyo itawasaidia namna ya kujiepusha na vitendo vya ukatili wa kijinsia, kuzingatia uzazi salama, kujikinga na magonjwa kama HIV pamoja na kuwajenga kisaiklojia ili kutambua bado wana nafasi ya kufikia ndoto na mafanikio yao katika jamii ambapo hadi sasa yametolewa kwa waraibu 30 jijini Mwanza ambapo lengo ni kuendelea kuwafikia waraibu wengi zaidi jijini Mwanza.

Naye Mkufunzi wa mafunzo hayo, Sophia Nshushi ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya Teens Corridor amesema waraibu wa dawa za kulevya wako kwenye hatari zaidi ya kupata magonjwa ya ngono ikiwemo HIV, mimba zilizotarajiwa na kuhisiwa kujihusisha na matukio ya uhalifu hivyo mafunzo hayo yatawapa mbinu zitakazowasaidia kujiepusha na mambo hayo na kurejesha imani katika jamii.

Baadhi ya waraibu wa dawa za kulevya akiwemo Feisal Seif na Mery’s Fabian wamesema makundi mabaya yaliwashawishi kuingia kwenye matumizi ya dawa hizo. Wamesema matumizi hayo yamewasababishia madhara makubwa kiafya na kimwili hivyo jamii hususani vijana ni vyema wakaepuka vishawishi vya kutumia dawa za kulevya.

“Mimi nilikuwa dereva wa magari makubwa (Excaveta) lakini baada ya kujiingia kwenye matumizi ya dawa za kulevya nilifukuzwa kazi, nimeamua kubadilika na kuacha na niko tayari kurejea kazini ikiwa nitapata tena kazi” amesema Seif.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Mkurugenzi wa Millagro Car Wash Esther Morris ambaye pia ni Mkurugenzi wa shirika la Naweza Tena akizungumza wakati wa semina ya kuwajengea uwezo waraibu wa dawa za kulevya jijini Mwanza ambapo ametoa rai kwa jamii kuwasaidia kupitia njia mbalimbali ikiwemo kuwapa kazi zisizohitaji ujuzi ili kuwaepusha na tamaa ya kujihusisha na uhalifu baada ya kukosa pesa kwa ajili ya kijikimu.
Mwanasaikolojia Paul Masele akitoa semina kwa waraibu wa dawa za kulevya jijini Mwanza.
Washiriki wakifuatilia semina hiyo.
Mwanasaikolojia Paul Masele akitoa semina kwa waraibu wa dawa za kulevya jijini Mwanza.
Mkufunzi wa mafunzo hayo, Sophia Nshushi ambaye ni Mkurugenzi wa taasisi ya Teens Corridor akitoa semina kuhusu ukatili wa kijinsia na afya ya uzazi kwa waraibu wa dawa za kulevya jijini Mwanza.
Washiriki wakifuatilia mafunzo hayo.
Picha ya pamoja.
Picha ya pamoja.
Itakumbukwa mradi wa uoshaji magari wa Millagro Car Wash jijini Mwanza unakenga kutoa fursa ya ajira kwa waraibu wa dawa za kulevya ili kujipatia kipato cha kujikimu kimaisha na kuanzisha miradi ya wenyewe hatua itakayosaidia kuingia kwenye tamaa ya kujihusisha na matukio ya uhalifu.

No comments:

Powered by Blogger.