LIVE STREAM ADS

Header Ads

MSD watakiwa kuendeleza mipango ya upatikanaji wa bidhaa za afya

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Pwani (RAS), Bi. Salvera Salvatory ameishauri Bohari ya Dawa (MSD) kuwa na mikakati endelevu ya kuboresha upatikanaji wa bidhaa za afya ili kuondoa malalamiko kwa wananchi ambayo kwa kiasi kikubwa yameanza kupungua.

Bi Salvatory ameyasema hayo wakati akifungua mkutano wa MSD Kanda ya Dar es Salaam na wadau wake wa Mkoa wa Pwani uliofanyika Kibaha Julai 6, 2023.

“Wananchi wanafarijika sana wanapofika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya wakapatiwa Dawa zote walizoandikiwa”

Kiongozi huyo amekiri kuvutiwa na MSD kuwa na kitengo cha Huduma kwa Wateja, ambao ndio hufanya mawasiliano kwa karibu na wadau na wateja, ambapo amewashauri kuhakikisha wanafuatilia malalamiko ya wateja na namna yanavyoshughulikiwa.

Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Miradi wa MSD Victor Sungusia ameeleza kuwa usambazaji wa bidhaa za afya mara sita kwa mwaka umesaidia kuongeza hali ya upatikanaji wa bidhaa hizo kwenye vituo vya kutolea huduma za afya nchini.

Kwa upande wake Meneja wa Kanda ya MSD Betia Kaema ameahidi kufanyia kazi maazimio yote yaliyoazimiwa kwenye kikao hicho huku akisisitiza ushirikiano na mawasiliano ya mara kwa mara na wadau hao.
Wadau wa MSD wakiwa kwenye mkutano huo
Mkutano ukiendelea
Kaimu Mkurugenzi wa Uendeshaji na Miradi wa MSD, Victor Sungusia akiwa kwenye mkutano huo
Wadau wakiwa kwenye mkutano huo.

No comments:

Powered by Blogger.