Wakuu wa taasisi za afya Nchi za SADC wakutana Dar
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Wakuu wa Taasisi zinazosimamia Manunuzi ya Bidhaa za Afya kwa nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukutana jijini Dar es Salaam jana Julai 10, 2023 katika mkutano wa siku tatu.
Na Mwandishi Wetu
Wakuu wa Taasisi zinazosimamia Manunuzi ya Bidhaa za Afya kwa nchi za SADC wamekutana jana Julai 10, 2023 jijini Dar es Salaam, kujadiliana na kuweka mikakati ya pamoja ya kuboresha mpango wa manunuzi ya pamoja ya bidhaa za afya kwa nchi za ukanda wa Kusini mwa Africa-SADC (SPPS).
Washiriki hao pamoja na mambo mengine watajadili namna bora ya kutekeleza mpango wa manunuzi ya pamoja ili kuweza kutekeleza mpango huo kwa ufanisi zaidi na kujadili mapendekezo yaliyotolewa na mshauri mwelekezi.
Nchi 16 Wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) ambazo ni wanachama wa mpango huo wa manunuzi ya bidhaa hizo za afya ni Angola, Boswana, Jamuhuri ya Demokrasia ya Congo, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Seychellers, Msumbiji, Namibia, Afrika ya Kusini, Eswatini, Tanzania , Zambia, Comoros, na Zimbabwe.
Mkutano huo wa siku tatu ulianza jana Julai 10, 2023 na utafikia tamati kesho Julai 12, 2023 kwa wakuu wa taasisi hizo kutembelea Bohari ya Dawa (MSD) Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika zikiwamo za uhifadhi wa dawa na vifaa tiba.
Mshiriki wa mkutano huo kutoka Zambia akiwa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea
Washiriki wa mkutano huo wakibadilishana mawazo
Washiriki wa mkutano huo kutoka Eswatini wakiwa kwenye mkuano huo.
Washiriki wa mkutano huo wakibadilishana mawazo
Mkutano huo ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Mkutano ukiendelea.
Washiriki wakifuatilia mawasilisho yaliyokuwa yakitolewa kwenye mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Washiriki kutoka Angola wakiwa kwenye mkutano huo.
No comments: