LIVE STREAM ADS

Header Ads

Kamati ya UKIMWI jijini Mwanza yaridhishwa na afua za kudhibiti VVU

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
 Kamati ya kudhibiti maambukizi ya UKIMWI inayoundwa na madiwani wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza imeridhishwa na afua mbalimbali za kudhibiti maambukizi hayo hususani kwa vijana ambazo ni pamoja na kuwajengea uwezo kiuchumi ili kuepukana na vishawishi.

Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mariam Mafutaa ameyasema hayo Ijumaa Agosti 18, 2023 akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati hiyo wakati wa ziara ya kukagua miradi ya UKIMWI.

Akizungumza wakati wa kukagua shughuli za ujasiriamali zinazofanywa na kikundi cha mabinti cha Tunaweza kilichopo Mkolani, Mafutaa amesema hatua ya mabinti hao kujengewa uwezo wa kujitegemea kiuchumi imewanusuru na vishawishi ambavyo vilikuwa vikisababisha kujiingiza kwenye tabia hatarishi zinazoweza kusababisha maambukizi ya VVU/ UKIMWI kuenea.

Mafutaa ameshauri kikundi hicho chenye mabinti zaidi ya 20 kuongeza jitihada za kuwafikia mabinti weni zaidi walio katika hatari ya kujiingiza kwenye vitendo hatarishi ikiwemo vya kingono na kuwaelimisha.

Pia Mafutaa amewahimiza mabinti wanaounda vikundi vya ujasiriamali ikiwemo kikundi cha Tunaweza kusajili vikundi vyao na kuomba mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na Halmashauri ili kuimarisha zaidi shughuli zao za ujasiriamali.

Mwenyekiti wa kikundi cha Tunaweza, Anipha Nassor amesema baada ya kikundi hicho kupatiwa mafunzo mbalimbali ya ujasiriamali na shirika la ICAP kupitia mradi wa Dreams wameweza kujikwamua kiuchumi na kujiepusha na vishawishi.

"Tunaomba Serikali kuweka mazingira ya kila Kata kuwa na eneo maalum kwa ajili ya vijana kufanya shughuli za ujasiriamali. Pia vijana wa kiume tunaomba wajiunge na mradi wa Dreams maana kwa sasa wanufaika ni mabinti tu, hiyo itasaidia mradi kuwa na manufaa zaidi" amesema Anipha.

Baadhi ya mabinti waliotoa ushuhuda wakati wa ziara hiyo wamesema mradi wa Dreams umewasaidia kujiepusha na utumikishwaji wa kingono na sasa wanajitegemea kiuchumi na hivyo kulishukuru shirikala ICAP kwa kuwajengea ujuzi.
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mariam Mafutaa akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI wakati wa ziara ya kutembelea kikundi cha mabinti cha Tunaweza kilichopo Mkolani.
Diwani wa Viti Maalum Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Mariam Mafutaa akizungumza kwa niaba ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI wakati wa ziara ya kutembelea kikundi cha mabinti cha Tunaweza kilichopo Mkolani.
Mwenyekiti wa kikundi cha mabinti wajasiriamali cha Tunaweza, Anipha Nassor akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Mwenyekiti wa kikundi cha mabinti wajasiriamali cha Tunaweza, Anipha Nassor akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Mmoja wa wanachama wa kikundi cha mabinti wajasiriamali cha Tunaweza, Ever Alloyce akisoma risala kwa wajumbe wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza pia imekagua huduma mbalimbali katika Hospitali ya Wilaya Nyamagana, Butimba na kuona jitihada mbalimbali zinazochukuliwa katika kudhibiti maambukizi ya VVU/ UKIMWI.
Wajumbe wa Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakiwasili katika Hospitali ya Wilaya Nyamagana, Butimba.
Kamati ya Kudhibiti UKIMWI kutoka Halmashauri ya Jiji la Mwanza wakikagua bidhaa mbalimbali zinazozalishwa na mabinti wajasiriamali kutoka kikundi cha Tunaweza ambao ni miongoni mwa vikundi takribani 18 vinavyojengewa uwezo na shirika la ICAP kupitia mradi wa Dreams ili kujiepusha na vihatarishi vya maambukizi ya VVU/ UKIMWI.
Picha ya pamoja.
PIA SOMA>>> HABARI ZAIDI HAPA

No comments:

Powered by Blogger.