LIVE STREAM ADS

Header Ads

Ujue kampuni ya mabasi Jostano Trans

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Mabasi ya Kampuni ya Jostano and General Supplises Limited yakiwa Stendi ya Mabasi ya Mkoa wa Singida Misuna tayari kwa safari zake.

Na Dotto Mwaibale, Dar es Salaam
Kampuni ya Jostano and General Supplises Limited licha ya kuanza kufanya kazi hivi karibuni imekuwa kinara katika sekta ya usafirishaji hapa nchini hususani katika Mikoa ya Singida, Manyara, Morogoro, Dar es Salaam, Dodoma na Mbeya.

Licha ya kuwa na miaka miwili katika sekta hiyo tangu ianze kufanya kazi zake mwaka 2021 kampuni hiyo imejizolea umaarufu mkubwa kutokana na utoaji wa huduma zake kwa viwango vya hali ya juu na kuwa kimbilio la abiria wengi.

Mfanyabiashara Margaret Ntandu ambaye anasafirisha mchele kati ya Mkoa wa Tabora kupitia Singida anasema amekuwa akisafirisha bidhaa hiyo kupitia mabasi ya kampuni hiyo na haja wahi kupata changamoto yoyote.

''Nimekuwa nikisafirisha mizigo yangu kutoka Singida kwenda Dodoma sijawahi kupata changamoto ya aina yoyote iwe ya kupotea mzigo na nyingine na hata bei zao ni rafiki ukilinganisha na mabasi ya kampuni zingine'' amesema Ntandu.

Edina Alex ambaye ni mfanyabiashara wa vitenge anayevitoa Tunduma na kuvipeleka Singida amesema mabasi ya kampuni hiyo ndiyo anayopanda wakati akifuata bidhaa zake hizo na kuwa wafanyakazi wa kampuni hiyo wamekuwa na lugha nzuri kwa abiria.

Alex amesema tangu kampuni hiyo ianze kufanya safari zake Mkoa wa Mbeya anatumia mabasi ya kampuni hiyo na akaupongeza uongozi kwa kusimamia vizuri utendaji kazi wa wafanyakazi ambao umewapa mafanikio hayo kwa kipindi kifupi tangu waingie kwenye sekta hiyo.

''Niwaombe viongozi wa kampuni hii waendelee kuwa wabunifu kwa kujifunza zaidi kutoka kwa makampuni yenye uzoefu naamini ndani ya miaka miwili ijayo Jostano Trans watakuwa wabobezi wakubwa kwenye sekta hii kwani wameanza vizuri'' amesema Alex.

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Amina Seif ambaye husafiri na basi la kampuni hiyo kutoka Singida kwenda Dar es Salaam amesema muda wanaoambiwa kufika Dar es Salaam kutoka Singida unakuwa ni uleule wa saa 11 na nusu jioni tofauti na mabasi mengine ambayo yanafika kuanzia saa 12 jioni hadi saa mbili na kuendelea.

''Abiria waliowengi hawapendi longolongo wanapenda kufika muda uleule walioambiwa labda tu ziwepochangamoto za kuharibika kwa gari lakini za kukamatwa na trafiki zinaweza kuepukika kwa kuzingatia sheria za usalama barabarani kama za mwendo kasi, uchakavu wa gari na matairi'' amesema Seif.

Amesema lugha nzuri wakati wa utoaji huduma kwa abiria ni jambo lingine ambalo limemfanya avutike na kusafiri kwa kutumia mabasi hayo na utaratibu wa kuomba dua wakati wa kuanza safari na baada ya kufika.

Wakala wa mabasi katika Stendi Kuu ya Mabasi Mkoa wa Singida aliyejitambulisha kwa jina la Awadhi Sendoro amesema amefanya kazi hiyo kwa muda mrefu katika stendi hiyo na kueleza kuwa kampuni hiyo kwa muda mfupi tangu ianze kufanya kazi imekuwa na wateja wengi.

''Mimi sio wakala wa mabasi hayo lakini kutokana na watu wengi kuwa na namba zangu wamekuwa wakinipigia simu niwashikie nafasi katika mabasi hayo na nimekuwa nikifanya hivyo'' amesema Sendoro.

Amesema abiria wengi wamekuwa wakipenda kusafiri na magari hayo kwa sababu ya huduma nzuri wanazozipata na kufika muda wanaoambiwa na mwendo mzuri wa mabasi hayo.

Katibu Mkuu Kiongozi wa Kampuni hiyo hiyo, Elias Meko amesema mafanikio hayo waliyoyapata kwa muda mfupi yanatokana na ushirikiano baaina ya viongozi wa kampuni hiyo pamoja na wafanyakazi ambao wakati wote ndio wanaokuwa na abiria.

''Tumekuwa tukikutana na wafanyakazi wetu wa kada zote wakiwemo makondakta na madereva na kufanyanao vikao kazi kwa ajili ya kukumbushana majukumu ambayo matunda yake ndiyo mafanikio haya yanayoonekana kwa abiria tunao wahudumia'' amesema Meko.

Amesema kampuni hiyo ilianza rasmi kufanya kazi zake mwaka 2021 kati ya Singida na Babati Manyara na baadae Singida, Dodoma, Morogoro na Dar es Salaam.

Meko amesema hivi sasa wameanzisha safari ya kutoka Singida kwenda Mbeya na kuwa kampuni yao hivi sasa imekuwa bora na kimbilio kwa wananchi wanaosafiri kwa mabasi yao.

Amesema licha ya kuwepo na ushindani wa kibiashara hali sio mbaya hasa ukizingatia kuwa hawana muda mrefu tangu waingie kwenye sekta hiyo na amewaomba wananchi kuendelea kuwaamini na kuwaunga mkono zaidi na wao wataendelea kuwapa ushirikiano lengo likiwa ni kuunga mkono jitihada za Serikali chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuhakikisha sekta ya usafirishaji inakua na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Meko amesema vitu vya kuzingatia kuwa ni vigezo na masharti vilivyowekwa ni nauli iliyowekwa kwenye tiketi haibadilishwi, kuzingatia muda wa safari na abiria afike kwenye kituo cha kupandia bus kabla ya nusu, mzigo wa ziada utakaozidi kilo 20 utatozwa nauli, mzigo wa mkononi wa abiria sio dhamana yao, abiria akisitisha safari atoe taarifa saa 12 kabla ya safari na atakatwa asilimia 15 ya nauli aliyolipa.

Ametaja vigezo na masharti mengine kuwa ni iwapo abiria atasitisha safari pasipo kutoa taarifa au kuachwa na basi kwa kuchelewa kufika kituo cha kupanda nauli haitarudishwa.

Amesema viongozi wa kampuni hiyo wapo tayari wakati wote kupokea maoni mbalimbali wanayoletewa na wasafiri wao na kuyafanyia kazi mara moja ikiwa ni ni moja ya njia ya kuboresha huduma zao.

Amesema kila penye mafanikio hapakosi kuwa na changamoto za hapa na pale hivyo aliwaomba wateja wao kuendelea kuwaamini na kwa changamoto zilizojitokeza wakati wa safari zao wanaomba wawasamehe,

Pia Meko ameendelea kuwahimiza wateja wao kukata tiketi kwenye ofisi zao au kwa njia ya mtandao jambo litakalosaidia kuondoa changamoto za kuzidishiwa nauli na kutapeliwa,

Katika hatua nyingine Meko amesema kampuni hiyo itakuwa na uchoyo wa fadhira iwapo itashindwa kumshuru na kuthamini mchango wa Kampuni ya mabasi ya Happy Nation katika mchango mkubwa wa ukuaji wa kampuni yao ya Jostano Trans na kuwa wanashirikiana viziri na Mkurugenzi wa kampuni hiyo ndugu Issa ambaye amekuwa hachoki kushiriukiana nao katika kila jambo la kuboresha utendaji kazi ambao umewaletea mafanikio hayo.
Wafanyakazi wa Basi namba T 133 DEA wakiwa mbele ya basi hilo tayari kwa safari ya Dar es Salaam kwenda Singida.Kushoto ni Dereva Hamad Athuman na kulia ni Kondakta Martha William.
Abiria wakiingia katika basi Stendi kuu ya mabasi Singida.
Wafanyakazi wa mabasi hayo wakiwa mbele ya moja ya mabasi hayo kabla ya kuanza safari. Kuitoka kushoto ni Kondakta wa mabasi hayo Martha William, Msimamizi wa Usalama na haki za abiria upande wa Dar es Salaam, Ally Atuman na kulia ni Ofisa Mwandamizi wa Ofisi ya kampuni hiyo Makao Makuu Dar es Salaam, Vanessa Samwel.
Basi la kampuni hiyo linalofanya safari zake kati ya Mbeya na Singida likiwa safarini.

No comments:

Powered by Blogger.