LIVE STREAM ADS

Header Ads

Rais Samia aridhishwa na utendaji MSD

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt .Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye ufunguzi wa Kikao Kazi kwa Wenyeviti wa Bodi na Watendaji Wakuu wa Taasisi za Umma kilichoandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina kwa kushirikiana na Jukwaa la Wakuu wa Taasisi za Umma, kilichofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa AICC Jijini Arusha tarehe 19 Agosti, 2023.
***

Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameridhishwa na mabadiliko yanayoendelea Bohari ya Dawa (MSD) na kuwataka waendeleee kuchapa kazi.

Rais Samia amesema hayo Jumamosi Agosti 19, 2023 jijini Arusha wakati akifungua kikao kazi cha wenyeviti wa bodi na taasisi za umma.

Rais Dkt. Samia akiwa amemsimamisha Mkurugenzi wa MSD, Mavere Tukai alisema taasisi hiyo ni kati ya mashirika yaliyo badilika na matumaini yake itakwenda kufanya vizuri hasa katika mfumo wa uuzaji wa Dawa Afrika kwa kuwa na soko kubwa hususani kwa nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara (SADC).

No comments:

Powered by Blogger.