LIVE STREAM ADS

Header Ads

Wananchi wafurahia huduma za RITA kwenye Maonesho ya Nanenane 2023

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano 0757 43 26 94 ama ripotabmg@gmail.com
Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Frank Kanyusi akimkabidhi cheti cha kuzaliwa mmoja wa wananchi kwenye maonesho ya kimataifa ya kilimo Nane Nane katika viwanja vya John Mwakangale Mkoani Mbeya
*****

Wananchi wameipongeza RITA kwa kutoa elimu, kufanya usajili na kutoa vyeti vya kuzaliwa kwenye maonesho ya kilimo Nane Nane 2023 katika viwanja vya John Mwakangale mkoani Mbeya.

Wamesema kuwa wamenufaika pakubwa kwa elimu kuhusiana wosia na mambo ya ndoa huku wakiisifu zaidi kwa kuwapatia vyeti vyao hapo hapo kwenye maonesho hayo.

"Mimi nimepata ruhusa ya siku mbili nikasema nikajaribu kufuatilia japo sikua na uhakika lakini nashukuru Mungu nmepata cheti changu hiki hapa sahizi naenda kuomba zangu Chuo" amesema Anita Mwakilasa.

"Siku zote huwa nasema nitaandika kesho, lakini nawapongeza hawa RITA wamenielimisha kwanza wosia sio uchuro na wosia ni siri, sasa nina amani na nitaenda waniandikie" ameongeza Stani Ngimba.

Aidha Kabidhi Wasii Mkuu na Afisa Mtendaji Mkuu wa RITA, Frank Kanyusi na Naibu Kabidhi Wasii Mkuu, Irene Lesulie wameshiriki kutoa huduma na kukabidhi vyeti vya kuzaliwa kwa wananchi katika banda la RITA wakati wa maonesho hayo.

No comments:

Powered by Blogger.