Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara afungua Maonesho ya 18 ya Biashara Afrika Mashariki
Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe amefungua Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na chemba ya wafanyabishara, wenye viwanda na kilimo (TCCIA) ambayo yanafanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Kigahe amefungua maonesho hayo Agosti 28, 2023 kwa niaba ya Waziri wa Biashara na Viwanda, Dkt. Ashatu Kijaji na kutumia fursa hiyo wafanyabiashara na wazalishaji wa bidhaa mbalimbali kutumia maonesho hayo kubadilishana uzoefu ili kuboresha bidhaa zao.
Kigahe amesema maonesho hayo pia yanayoa fursa kwa wafanyabishara, wajasiriamali na makampuni mbalimbali kutoka nchi za Afrika Mashariki kuonyesha bidhaa zake, kujitangaza na kukuza soko la biashara kupitia soko huru la Afrika Mashariki.
Naye Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa Mwanza, Gabriel Kenene amesema maonesho hayo yanatoa fursa kwa wafanyabiashara Afrika Mashariki kutangaza biashara zao na kupata masoko mapya. Hata hivyo Kenene ameomba mamlaka za Serikali kuweka mazingira rafiki na rahisi mipakani ili kuondoa adha kwa wafanyabiashara wanaoshiriki maonesho hayo.
Katika maonesho hayo, pia wadau kutoka taasisi mbalimbali za umma na binafsi zimetumia fursa hiyo kutoa elimu kwa wananchi ambapo miongoni mwa wadau hao ni Wakala wa Usajili, Biashara na Leseni (BRELA) ambao wamejikita kuelimisha wananchi kutambua umuhimu wa kusajili biashara zao.
Akizungumza kwenye maonesho hayo, Afisa Habari wa BRELA, Gloria Mbilimonywa pia watatua fursa ya maonesho hayo kutoa huduma mbalimbali ikiwemo usajili wa alama za biashara, majina ya biashara na makampuni ya biashara na hivyo kutoa rai kwa wananchi kutembelea banda la BRELA.
Kwa mara ya kwanza maonyesho ya biashara ya Afrika Mashariki yanayoandaliwa na TCCA yalianza mwaka 2006 ambapo kwa mwaka huu ni mara ya 18 kufanyika yakianza Agosti 25 hadi Septemba 02 yakiambatana na kaulimbiu isemayo " mazingira bora ya biashara ni kivutio cha kukuza uwekezaji wa biashara, kilimo na viwanda Afrika Mashariki".
Na George Binagi- GB Pazzo, BMG
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Viwanda na Biashara, Dkt. Ashatu Kijaji (hayuko pichani) kwenye ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na TCCIA uliofanyika Agosti 28, 2023 kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa Mwanza, Gabriel Kenene akizungumza wakati wa ufunguzi wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Afisa Habari BRELA, Gloria Mbilimonywa (kulia) akitoa ufafanuzi kwa Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe (kushoto) kuhusu huduma zinazotolewa na taasisi hiyo kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika kwenye uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe (kushoto) akiwa kwenye banda la BRELA wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika katika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza.
Wananchi na wadau mbalimbali wakipata elimu katika banda la BRELA kwenye Maonesho ya 18 ya Biashara ya Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na TCCIA.
Katibu wa CCM Mkoa Mwanza, Omary Mtuwa (kulia) akipata ufafanuzi wa huduma mbalimbali zinazotolewa na BRELA alipotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 18 ya Biashara ya Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na TCCIA.
Katibu wa CCM Mkoa Mwanza, Omary Mtuwa (kulia) akipata ufafanuzi wa huduma mbalimbali zinazotolewa na BRELA alipotembelea banda la taasisi hiyo wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 18 ya Biashara ya Afrika Mashariki.
Maafisa wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) wakiwa kwenye Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki yaliyoandaliwa na TCCA.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa Mwanza, Gabriel Kenene (katikati) akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara na, Exaud Kigahe (kushoto) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 18 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza kuanzia Agosti 25 hadi Septemba 02, 2023.
Mwenyekiti wa TCCIA Mkoa Mwanza, Gabriel Kenene (kulia) akimkabidhi zawadi Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe (kushoto) wakati wa ufunguzi wa Maonesho ya 18 ya Biashara ya Afrika Mashariki yanayofanyika uwanja wa Furahisha jijini Mwanza kuanzia Agosti 25 hadi Septemba 02, 2023.
SOMA PIA>>> HABARI ZAIDI HAPA
No comments: