LIVE STREAM ADS

Header Ads

Msukuma awasha moto jimboni, ataka fedha za Wavuvi zirudi

Yaliyomo humu (Habari, Matangazo na Maoni) si msimamo wa BMG Media. Mawasiliano +255 757 432 694 ama ripotabmg@gmail.com


Mbunge wa Jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku Musukuma (kulia aliyeshika barua) akizungumza na Wavuvi wa Mwaro wa Makatani Kata ya Nkome wilayani Geita ambao wanalalamikia kutozwa faini kinyume na utaratibu.

Na Victor Bariety Geita
Mbunge wa Jimbo la Geita vijijini Joseph Kasheku Musukuma ameuagiza uongozi wa BMU Mwaro wa Makatani uliopo Kata ya Nkome wilayani Geita kurejesha fedha zaidi ya Sh.400, 000 walizochukua kwa baadhi ya wavuvi wa mwaro huo ambazo waliwatoza kama faini ya kuvua dagaa wakati wa giza kinyume cha utaratibu.

Mbunge Musukuma ametoa agizo hilo alipofanya ziara ya kushitukiza kwenye mwaro huo kisha kuzungumza na wavuvi wa eneo hilo ambapo bila kumung'unya maneno wavuvi hao walimweleza mbunge wao kuwa uongozi wa BMU kata hiyo wamekuwa wakiwanyanyasa Kwa kuwatoza faini zisizo rafiki pasipo hata kuwapatia risti za malipo hayo.

"Baadhi ya viongoz wa BMU hapa makatani wanatunyanyasa sana na wamekuwa wakituzuia kuvua dagaa majira ya giza lakini pia wanapotukamata wanatutoza faini ya shilingi elfu hamsini na hatupewi risiti ya malipo hayo" alisema Mussa Juma huku akishangiliwa na wavuvi wenzake na kuongeza mfano juzi tumekamatwa na tumetozwa faini ya Sh.50,000 kila mmoja na hatukupewa risti".

Kufuatia malalamiko hayo Mbunge Musukuma ametaka kupata ufafanuzi kutoka kwa uongozi wa kijiji hicho ña kuelezwa KUWA agizo hilo limetoka Kwa uongozi Wa Halmashauri hiyo lengo likiwa ni kuokoa mazalia ya samaki".

"Siyo kwamba tumejiamulia kuwakamata hawa wavuvi ni agizo kutaka Kwa Mkurugenzi wa Halmashauri na lengo ni kufanya samaki wazaliane"amesema Mtendaji wa Kata ya Nkome, John Nzari.

Hata hivyo baada ya maelezo hayo kutoka kwa Mtendaji, Musukuma amepitia barua iliyotoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo inayoelekeza utekelezaji wa agizo hilo na kuhoji iwapo kwenye barua hiyo wameagizwa kuwatoza faini wavuvi hao pasipo kupatiwa risti lakini nakupata majibu yanayojitosheleza.

"Ni kweli hii barua imewaelekeza kukamata wavuvi wanaovua dagaa nyakati za Giza lakini ni wapi ambapo imeelekeza muwatoze faini pasipo kuwapatia risti?" amehoji Musukuma

kufuatia hali hiyo mwenyekiti wa BNU Kata hiyo, Ntuzu Emmanuel amejitetea kuwa walikuwa na mpango wa kuwaita wavuvi hao ili wawapatie risti zao uteteziambao pia uligonga mwamba kwa mbunge huyo na kuamuru pesa hiyo irejeshwe haraka Kwa wavuvi hao na iwe mwanzo na mwisho kuwatoza wavuvi hao pesa zao pasipo kuwapatia risti.

"Nataka pesa mliyochukua kwa wavuvi muirejeshe mara moja na iwe mwanzo na mwisho kuwatoza faini pasipo kuwapatia risti, mnasikia nyie wavuvi msikubali kutoa pesa bila kupewa risti hata serikali inasisitiza unapofanya malipo ya aina yoyote ile dai risti" alisema mbunge Musukuma huku akipigiwa makofi

Kufuatia hali hiyo uongozi huo wa BMU umemhakikishia mbunge Msukuma kuwa pesa yote watairejesha na kwamba suala hilo halitajitokeza tena.

Katika hatua nyingine wavuvi hao walimtaka mbunge huyo kuondoka na mtendaji wa Kijiji hicho Salum Mussa Kapami kwa madai amekuwa ni mungu mtu.

"Mbunge uondoke na mtendaji wa Kijiji amekuwa amekuwa Mungu mtu tunaomba uondoke naye" amesema Geradi Masaga huku akishangiliwa na wavuvi wenzake.

Aidha, akijibu malalamiko hayo Musukuma amemtaka mtendaji huyo kujibu hoja za wavuvi hao na kudai kuwa anasingiziwa

"Ninakuomba ujirekebishe ukiendelea hivyo nitaongea na mkurugenzi akuondoe maana wameshaondoka watendaji wengi sana hapa ambao hawawezi kutatua kero za wananchi" amesema Musukuma.
Ukutano na wavuvi ukiendelea.
Barua kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Geuta ikisomwa na kuoneshwa katika mkutano huo.

No comments:

Powered by Blogger.